Timu
ya Taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 17 (Serengeti Boys) itacheza na
Afrika Kusini katika mechi za mchujo kutafuta tiketi ya kucheza Fainali za
Afrika kwa umri huo zitakazofanyika mwakani nchini Niger.
Serengeti
Boys ambayo pamoja na nchi nyingine 17 zimeingia moja kwa moja katika raundi ya
pili itaanzia mechi hiyo nyumbani kati ya Julai 18-20 mwaka huu wakati ile ya
marudiano itafanyika nchini Afrika Kusini kati ya Agosti 1-3 mwaka huu.
Ikifanikiwa
kuitoa Afrika Kusini, Serengeti Boys itacheza mechi ya raundi ya tatu na ya
mwisho na mshindi wa mechi kati ya Misri/Sudan vs Congo Brazzaville.
Nchi
nyingine ambazo zimeingia moja kwa moja raundi ya pili ni Afrika Kusini, Angola,
Benin, Botswana, Burkina Faso, Congo Brazzaville, Ethiopia, Gabon, Ghana, Ivory
Coast, Mali, Morocco, Nigeria, Rwanda, Senegal, Tunisia na Zambia.
Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) inatarajia kutangaza benchi la ufundi
litakaloiongoza Serengeti Boys hivi karibuni.
No comments:
Post a Comment