Karim Benzema na Franck Ribery matatizoni kwa kubaka |
Wachezaji wawili wa kandanda wa timu ya taifa ya Ufaransa Franck Ribery na Karim Benzema wameshtakiwa mahakamani hii leo mjini Paris kwa kutoa malipo ili kushiriki ngono na kahaba mwenye umri mdogo
Mshambuliaji wa Bayern Munich Ribery na mwenzake wa Real Madrid Karim
Benzema wanakabiliwa na adhabu ya hadi miaka mitatu gerezani na faini ya
juu ya kiasi cha euro 45,000 kama watapatikana na hatia ya uhalifu huo.
Wachezaji hao wote wawili wanakanusha mashtaka, na msichana
aliyehusika, Zahia Dehar, ametoa ushahidi kuwa wanasoka hao wawili
hawakujua kuwa alikuwa na umri wa chini ya miaka 18 wakati walipofanya
naye kitendo cha ngono mwaka wa 2008 na 2009.
Ijapokuwa umri unaoruhusiwa kisheria nchini Ufaransa wa mtu kuwa na
ufahamu ni miaka 15, kumlipa yeyote mwenye umri wa chini ya miaka 18,
ili kushiriki naye ngono ni uhalifu. Dehar kwa sasa na umri wa miaka 21.
Ribery mwenye umri wa miaka 30, alikiri kufanya mapenzi na Dehar,
lakini anasisitiza kuwa hakujua kuwa alikuwa na umri mdogo. Benzema naye
anakanusha kabisa kufanya kitendo hicho.
Ribery na Benzema hawakustahili kufika mahakamani, huku wakili wa Ribery
akisema kuwa kesi hiyo haikuwa na “mwathriwa”, ikizingatiwa kuwa Dehar,
aliondoa mahakamani malalamishi yake na “bila mashitaka yoyote”.
Waendesha mashtaka wa serikali waliitaka mahakama hiyo ya Paris itupilie
mbali kesi hiyo, wakihoji kuwa wanasoka hao wawili hawakujua kuhusu
umri wa Zahia wakati wa uchunguzi wa mwanzo. Jaji hata hivyo aliamua
kuwacha kesi hiyo wazi, akisema walistahili kuwa na uwezo wa kutambua
kuwa msichana huyo alikuwa na umri mdogo. Kesi hiyo inastahili kudumu
kwa takriban wiki moja, na hukumu yoyote huenda ikachukua muda mrefu.
Alberto Carlo Brusa, mwanasheria wa Bayern Munich akiwasili mahakamamni mjini Paris.
Zahia Dehar alifanya kazi ya ufuska wakati akiwa umri mdogo.
Zahia Dehar pichani juu amedai hakumuambia mteja wake kuwa alikuwa na umri mdogo.
No comments:
Post a Comment