Moyes kuanza kampeni dhidi ya Chelsea na Liverpool ndani ya michezo ya mwanzo ya ligi |
Mchezo wa kwanza wa meneja mpya wa Manchester United David Moyes katika uwanja wa nyumbani Old Trafford utakuwa ni dhidi ya kikosi cha meneja mpya wa Chelsea Jose Mourinho Chelsea.
Mabingwa hao wa Barclays
Premier League wataanza kampeni ya kutetea taji kwa kuwafuata Liverpool na Manchester City ndani ya michezo mitano ya kwanza ya msimu.
United
watafungua msimu dhidi ya mabingwa wa taji la ligi Swansea mchezo ambao umepangwa kufanyika Agosti 17, kabla ya kurejea na kucheza na kucheza Old Trafford kukumbana na kikosi cha Mourinho cha Chelsea wiki itakayofuata.
Mchezo dhidi ya United dhidi ya Liverpool utafuata Agosti 31 kabla ya mchezo dhidi ya Manchester City katika mchezo wao wa tano wa msimu Septemba 21.
Michezo ya ufunguzi wa msimu ya ligi ya England Agosti 17
Arsenal v Aston Villa
Chelsea v Hull City
Crystal Palace v Tottenham Hotspur
Liverpool v Stoke City
Manchester City v Newcastle United
Norwich City v Everton
Sunderland v Fulham
Swansea City v Manchester United
West Bromwich Albion v Southampton
West Ham United v Cardiff City
Soma ratiba kamili upenda wa kulia......................
Bingwa Man United itakuwa na kazi ya msimu mpya chini ya David Moyes
No comments:
Post a Comment