West Ham United imekamilisha zoezi la kumsajili mshambuliaji wa kimataifa wa England Andy Carroll kutoka klabu ya Liverpool kwa ada ya uhamisho ya rekodi ya klabu hiyo ya pauni milioni £15.
Carroll mwenye umri wa miaka 24, aliigharimu Liverpool kiasi cha pauni milioni 35 lakini baadaye akaaelekea kwa mkopo katika klabu ya West Ham mwezi Agosti ambako aliifungia jumla ya mabao saba katika jumla ya michezo 24 aliyoichezea klabu hiyo.
Mshambuliaji huyo wa zamanin wa Newcastle United amesaini mkataba wa miaka sita huku akipewa nafasi ya kuongeza miaka miwili hapo baadaye.
Amenukuliwa Carroll akisema
"N ivizuri kwangu kuwa hapa. Kwakweli nimefuhia msimu uliopita, na hii imedhihirisha kwa kuongeza mkataba wa kudumu".
No comments:
Post a Comment