Shirikisho la soka la Togo TFF limekiri kumtumia mchezaji si ambaye hakuwa halali kumtumia katika mchezo wao wa hatua ya makundi kuwania kufuzu kutinga hatua ya pili ya mtoano ya kombe la dunia lakini wametaka shirikisho la soka duniani kutoiadhibu.
Mjumbe wa tff Toussa Komi Gabriel amesema kuwa ni kweli Alaixys Romao hakupaswa kucheza katika mchezo wao dhidi ya Cameroon ambao walishinda kwa mabao 2-0 mjini Lome June 9.
Amenukuliwa akisema
"Ni kweli timu ya Togo haikugundua kuwa mchezaji wao hakuwa sthili kutumika katika mchezo huo tangu kabla "
Pia ametaka Togo isiadhibiwe na fifa kutokana na kujikanganya kwao adhabu ambayo ni kupoteza alama tatu.
Kauli ya kukiri ya Komi imekuja masaa machache baada ya Ethiopia kukiri kumtumia mchezaji ambaye hakuwa halali kama ilivyokuwa kwa Togo katika mchezo wao dhidi ya Botswana uliopigwa June 8.
Endapo alama za Togo zitapewa Cameroon, itarejeshea Indomitable Lions uhai wa kufuzu kwa hatua ya pili ya mtoano ya kuelekea kufuzu kombe la dunia.
Cameroon kwasasa wako nyuma ya kwa alama mbili dhidi ya vinara Libya katika kundi I na huenda alama hizo zikawapa uongozi wa kundi huku wakisaliwa na mchezo mmpja.
Timu 10 za kwanza pekee kutoka kila kundi zitaingia katika hatua ya pili ya mtoano ambapo michezo miwili ya nyumbani na ugenini itaamua ni timu zipi tano zitakuwa zimefuzu kwa safari ya kombe la dunia nchini Brazil 2014.
Sheria ya michuano ya kombe la dunia inasema mchezaji atakae pewa kadi mbili za njano katika michezo ya kampeni ya kufuzu atakuwa moja kwa moja anasimama kwa mchezo mmoja.
Africa imekuwa na kesi nyingi za utovu wa nidhamu na hivyo kukabiliwa na adhabu ya Fifa katika kampeni hizi za kuelekea kombe la dunia 2014.
Burkina Faso na Gabon zilipoteza alama kwa kuwachezesha wachezaji wazaliwa wa Cameroon ambao walikosa uhalali wa kutumikia timu hizo za taifa ilhali Sudan ilipoteza alama kwa kumtumia mchezaji ambaye alisimamishwa kwa kadi.
Ipo pia kesi inayoihusu Equatorial Guinea
ambayo ilitumia wachezaji kutoka Brazil na Colombia.
No comments:
Post a Comment