Kiungo mchezeshaji wa Arsenal aliye katika wakati mgumu kwasasa, kwa lugha ya kimombo 'Under-fire' Mesut Ozil, amepata pumzi ya faraja kufuatia meneja wake Arsene
Wenger kuweka wazi kuwa kiungo huyo ataendelea kupiga mikwaju ya penati licha ya kukosa kufunga mara mbili hivi karibuni.
Ozil amekuwa akisemwa sana midomoni mwa mashabiki wa Arsenal kufuatia kukosa penati katika mchezo muhimu wa hatua ya mtoano ya 16 bora dhidi ya Bayern
Munich katikati mwa juma.
Mjerumani huyo alipewa zawadi ya pigo la penati kufuatia kufanya jitahada kubwa za kujaribu kupata nafasi ya kufunga lakini upigaji wake wa pigo hilo haukuweza kuzaa goli ambalo pengine lingewapa bao la uongozi dhidi ya kigogo cha ligi kuu ya Ujerumani Bundesliga, Bayern Munich.
Hii ilikuwa ni mara ya pili kwa Ozil kukosa penati ya maguu 12 msimu huu, ambapo alikosa penati kwa mara ya kwanza katika mchezo dhidi ya Marseille, ilhali pia anaonekana kuwa katika kiwango kibovu tangu wakati huo akiwa na Real Madrid.
Wakati hayo yakiwa hivyo, mwa kujibu wa gazeti la Telegraph, ambalo lilimuuliza Wenger kama ataendelea kumpa nafasi ya kupiga tena penati, Wenger amesema atafanya hivyo huku akitolea mfano kwa nyota wa Bayern Arjen Robben na Bastian Schweinsteiger.
Wachezaji hao wote walikosa penati katika mchezo wa fainali ya ligi ya mabingwa Ulaya kabla ya kurejea vizuri na kuipa timu yao taji msimu uliofuata.
Wenger hakuwa tayari kumkosoa Ozil kwa kukosa kwake penati katika ya wiki, licha ya wenzake Lukas Podolski na Per
Mertesacker kuonekana kumzonga wakati wa mchezo.
No comments:
Post a Comment