Kocha
Msaidizi wa Taifa Stars, Sylvester Marsh ambaye amelazwa Hospitali ya Taifa
Muhimbili (MNH) anasubiri vipimo vya mwisho ili aweze kuanza matibabu.
Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limemhamisha kocha huyo kutoka nyumbani kwake jijini Mwanza na kumleta Dar es Salaam kwa lengo la kuhakikisha anapata matibabu zaidi
na kwa uangalizi wa karibu.
Tayari
majibu ya kipimo cha kwanza yameshapatikana, hivyo yanasubiriwa majibu ya
kipimo kingine ili aweze kuanza rasmi matibabu, lengo likiwa ni kubaini
kitaalamu ugonjwa unaomsumbua.
No comments:
Post a Comment