Alhaji Msafiri Ahmed Mgoyi ataiongoza Twiga Stars nchini Zambia |
Kikosi cha Twiga kikiendelea na maandalizi yake. |
Timu
ya Twiga Stars itaagwa rasmi Jumatano (Februari 12 mwaka huu) tayari kwa safari
ya Lusaka, Zambia kwa ajili ya mechi ya kwanza ya raundi ya pili ya michuano ya
Afrika kwa Wanawake (AWC) ambayo fainali zake zitafanyika Oktoba mwaka huu
nchini Namibia.
Msafara
wa timu hiyo itakayoondoka kwa ndege ya Fastjet utaongozwa na mjumbe wa Kamati
ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Ahmed Idd Mgoyi.
Hafla
ya kuwaaga wachezaji wa timu hiyo itafanyika saa 5 asubuhi kwenye ofisi za TFF.
Timu hiyo itaondoka Februari 13 mwaka huu alfajiri tayari kwa mechi hiyo
itakayochezeshwa na waamuzi kutoka Rwanda.
No comments:
Post a Comment