KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Wednesday, February 12, 2014

Roy Hodgson amemaliza ndoto za John Terry za kurejea katika kikosi cha timu ya taifa ya England

Roy Hodgson amemaliza ndoto za John Terry za kurejea katika kikosi cha timu ya taifa ya England katika michuano ya kombe la dunia.
Kocha huyo mkuu wa England kwa mara nyingine tena amethibitisha kuwa mlizni huyo aliye majeruhi hatakuwa katika kikosi chake katika michuano hiyo ya majita ya kiangazi nchini Brazil.
Terry ambaye alistaafu kucheza kikosi hicho kwa hiari yake October 2012 amekuwa ni mlinzi wa kiwango kizuri cha kuvutia katika Barclays Premier League msimu huu.

Ingawa Terry mara zote amekuwa akikaririwa kuwa hana mapango wa kurejea tena kikosini England kumekuwepo na nguvu ya nje ambayo imekuwa ikimtaka kurejea kikosini kwa ajili ya fainali hizo za barani America ya kusini.
Hata Hodgson amekaririwa akisema
‘Sina la kusema zaidi ya kile nilichokisema . John amestaafu na kwa kuwa hili linanihusu basi hali ya halisi ndiyo hiyo.
‘Tumekuwa tukisonga mbele bila ya yeye katika kipindi chote cha harakati za kuwani kufuzu na katika michezo michache ya kirafiki hivyo basi hatutakuwa naye hapo baadaye.

Kwa mara ya mwisho kuwepo katika kikosi cha England ilikuwa ni katika mchezo wa kuwani kufuzu dhidi ya Moldova mwezi  September, 2012 akiwa na michezo 78 na akiwa na magoli sita.

No comments:

Post a Comment