Mwamuzi wa
zamani wa ligi kuu ya soka nchini Afrika kusini Andile ‘Ace’ Ncobo amezungumzia
juu ya presha inayowakumba waamuzi wa mchezo mkubwa utakao pigwa Jumamosi mjini
Soweto maarufu kama Soweto Derby baina ya Orlando Pirates dhidi ya Keizer
Chiefs.
Ncobo ambaye
pia ni meneja wa zamani wa PSL amesema katika soka nchini Afrika kusini hakuna
kama Soweto Derby na kwamba jambo pekee ambalo litawasaidia waamuzi hao katika
mchezo huo mkubwa nchini Afrika kusini ni kuwa vizuri kiakili(mentally tough).
“Uzoefu ni
kitu bora, ni mchezo mkubwa katika kalenda ya soka la nchi hiyo bila kujali ni
mchezo wa ligi, wa michuano tu, wa kirafiki, mchezo wa nje ya msimu yaani bado
ni mchezo mkubwa”Ncobo alikuwa akiongea na SuperSport katika mahojiano.
“Najua makamishina
wa mchezo na waamuzu watawaambia waamuzi hao kuuchukulia kama michezo mingine,
lakini ukweli ni kwamba si kama michezo mingine.
“Unakuja na
presha kubwa, na ni presha hiyo ndiyo inayoingia ndani, hutarajii nini
kitatokea katika mchezo, huwezi kwa kweli kujiandaa , unachotakiwa ni kuwa
imara kiakili.”
Orlando
Pirates na Kaizer Chiefs watapambana Jumamosi uwanja wa FNB Jumamosi mchana.
Gary
Neville amtolea uvivu Asern Wenger kuhusu Ozil
Gary Neville amemtolea uvivu meneja wa
Arsenal Arsene Wenger kwa kushindwa kumpa muda wa kupumzika nyota wake Mesut
Ozil katika kipindi cha mwisho wa mwaka yaa kipindi cha sikukuu za krismass na
mwaka mpya ambapo alitolea mfano Cristiano Ronaldo mara kadhaa alikuwa akipewa
mapumziko ya kipindi cha mapumziko nyakati kama hizo wakati huo akiwa na Sir
Alex Ferguson enzi zake ndani ya United.
Ozil sasa anatarajia kuanza
mapimziko ya wiki chache baada ya baada ya kukumbwa na matatizo ya msuli hapo
jana katika mchezo wa ligi ya ambingwa Ulaya dhidi ya ambapo walitolewa rasmi
mashindano usiku wa jana.
Kiungo huyo mjerumani alikuwa akionekana
kufanya vema katika mchezo muhimu wa robo fainali ya FA ambapo Arsenal walishinda
bao 4-1 dhidi ya Everton Jumamosi lakini amekuwa akilalamikiwa kwa kutojituma
katika michezo mikubwa tangu kuanza kwa mwaka.
Neville ametumia mtandao wake wa
kijamii wa Twitter kuweka wazi mawazo yake juu ya maamuzi ya Wenger kuendelea
kumtumia Ozil katika kipindi chote cha krismass.
Ujumbe wake wa mtandaoni umesomeka
'Mwili wake unaonyesha wazi kuwa
amekuwa akipambana ilhali akili ikiwa imechoka, hata hivyo ni jambo zuri kwani
atakapo rejea atakuwa na nguvu mpya!
FA ya Sierra Leone kuchunguza ugomvi Rais wa soka nchini humo Johansen na nahodha wa zamani Kallon
Chama cha soka nchini Sierra Leone (SLFA)
linajipanga kufanya uchunguzi juu ya sakata la baina ya Rais wa chama hicho Isha
Johansen na nahodha wa zamani wa nchi hiyo Mohamed Kallon.
Maamuzi hayo yanakuja siku moja
baada ya Kallon mwenye umri wa miaka 34,kushikiliwa na polisi kwa takribani masaa saba kwa mahojiano kabla
ya kuachiwa baada ya kutoa dhamani ya dolari za kimarekani $11,000.
Tukio hilo lilitokea machi 6 baada
ya mechi ya mchezo wa FA iliyohusisha timu ya Kallon, FC Kallon Junior, mjini Freetown.
Nyota huyo wa zamani wa Inter Milan na
Monaco, Kallon alilalamikia kuchapwa kibao kwa nyuma ya shingo na Johansen baada
ya mchezo.
Johansen baadaye akalalamika kuwa
alikuwa akijitetea kuwa alikuwa katika hali ya kujitetea baada ya kusukumwa na Kallon
ambaye pia alimtukana.
Kallon alipeleka lalamiko polisi
lakini Jumatatu alishikiliwa kwa mahojiano chini ya inspekta msaidizi wa pilisi
Al Sheikh Kamara ambaye alisema kuwa mchezaji huyo wa zamani alikuwa na tuhuma
za kujibu juu ya hilo.
On Wednesday, the SLFA released a
statement saying the matter had been referred to its disciplinary board. BBC
Sport understands that the SLFA executive committee has also recommended for
the matter to be dropped by police and dealt with by the governing body.
Baada ya Kallon kuhijiwa na polisi,
wakili wake Emmanuel Saffa Abdulai alikaririwa akisema
"nimeshangazwa na kushitushwa
na maamuzi ya polisi kumshikiliwa Kaloon, hili ni jambo la kushangaza kwakuwa
mteja wangu ndiye aliyepaswa kuwa mlalamikaji sio mlalamikiwa katika tukio hili
kwasababu yeye ndiye aliyepigwa kofi na ndiye alikuwa wa kwanza kushitaki
polisi juu ya jambo hili.
"Mteja wangu amefanyiwa
visivyo, mfumo huu wa sheria wa Sierra Leone unawapendelea wenye pesa."
Johansen amekataa kutoa maoni yake
kwakuwa sahauri hilo liko kwenye uchunguzi wa polisi.
Kumekuwepo na mahusino mabovu baina
ya Kallon na Johansen tangu uchaguzi wa SLFA uliofanyika mwaka 2013. Wawili hao
waliteuliwa kwa ajili ya kinyang’anyiro cha uchaguzi wa Urais kabla ya Kallon na
mgombea mwingine Rodney Michael kuenguliwa kwa kile kilechoitwa kuwa ni kukosa
sifa kwa mujibu wa kamati maalum fifa ambapo baadaye Johansen alichaguliwa bila
kupingwa.
Balotteli kikaaangoni Milan kiwango champonza
Mshambuliaji wa AC Milan Mario
Balotelli ameingia katika lawama nzito kutoka kila upande wa vyombo vya habari
vya Italia kufuatia kiwango chake kibovu katika michezo yote miwili ya klabu
bingwa ulaya dhidi ya Atletico Madrid .
Bingwa mara saba wa vilabu binngwa
Ulaya walitolewa katika michuano ya hiyo baada ya kufurushwa kwa kichapo cha
mabao ya jumla 5-1 na Atletico Madrid, ambao waliwachapa Milan bao 4-1 hapo
jana usiku.
The Gazzetta dello Sport lilimkosoa Balotelli
baada ya kushindwa kuonyesha ubora wake katika michezo yote miwili likiwa na
kichwa cha habari "Balotelli remains switched off,'' .
The Corriere dello Sport likiandika
"Terrible performance by the
Rossoneri. Kaka goal, Balotelli disaster.''
Clarence Seedorf, ambaye alichukua
kazi ya kuinoa Milan mwezi January baada ya kufukuzwa mtangulizi wake Massimiliano
Allegri, pia ameingia katika ulingo mbaya wa ‘under fire’.
Safu ya tahariri ya Gazzetta dello
sports imekuwa akilalamikia juu ya mbinu za ufundishaji za Seedorf na tabia ya Balotelli
kimchezo likisema "Balotelli and
Seedorf are also under scrutiny yaani wako chini ya uangalizi.''
No comments:
Post a Comment