KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Saturday, March 22, 2014

Mshambuliaji wa zamani wa Chelsea Adrian Mutu anajipanga kushindi wimbo mpya wa Snoop Dogg

Mshambuliaji wa zamani wa Chelsea Adrian Mutu amethibtitisha kuwa anajipanga kushiriki katika video mpya ya wimbo wa nyota wa musiki wa Hip Hop duniani Snoop Dogg.

Mutu, ambaye alifukuzwa katika klabu ya Chelsea mwaka 2004 baada ya kushindwa katika vipimo vya matumizi ya madawa kwasasa ana umri wa miaka 35 na anacheza katika klabu moja ya huko nchini Romania ya Petrolul Ploiesti.

Hata hivyo inaonekana kama mshambuliaji huyo anajipanga kuachana na soka na kujikita katika biashara ya muziki.

Taarifa za wiki iliyopita zinasema mwamuziki Snoop Dogg anatarajiwa kutoa video ya wimbo wake mpya na kumshirikisha mchezaji huyo kama sehemu ya kuimarisha mahusiano yao.
Big Day Out 2014 - Auckland
Snoop Dogg
Mutu amethibitisha taarifa hizo kupitia mtandao wake wa kijamii wa Instagram akichapicha picha iliyokuwa na ujumbe wa habari hiyo.

Mkurugenzi Massimo Caroletti,ambaye anafanya kazi karibu na Snoop, amewaambia wana habari kuwa Mutu anavutia sana kuwemo ndani ya video hiyo na kudokeza kuwaalikuwa tayari kumjumuisha mshambuliaji huyo katika kazi hiyo inayokuja.

No comments:

Post a Comment