Wayne Rooney anadai kuwa mchezaji ambaye amepewa kipau mbele kuzuiwa kuelekea kwenye mchezo wa kesho baina ya Manchester
United dhidi ya Liverpool si mwingine bali ni Luis Suarez mchezaji ambaye anatazamwa kuwa ni miongoni mwa wachezaji bora duniani kwasasa.
United
imekuwa ikifurahia ubora dhidi ya wapinzani wao hao wa zamani, katika kipindi cha karibu miongo miwili lakini msimu huu mambo yakiwaendea kombo kwani wameachwa nyuma katika msimamo wa ligi na wapinzani wao hao kutoka pande za Merseyside kwa alama 11 na ambao kwasasa wako katika nafasi ya pili katika msimamo wa Barclays Premier League.
Ukiangalia hali ya ididi ya ufungaji inaonyesha kuwa meneja wa Liverpool Brendan Rodgers ni kwamba anaonekana kufurahia mafanikio zaidi ya mwenzake wa upande wa pili David Moyes.
Liverpool imefunga jumla ya magoli 73 msimu huu ukilinganisha na United iliyoweka wavuni jumla ya magoli 46.
Mshambuliaji wa Liverpool
Suarez, ambaye ameimarisha muunganiko mzuri wa safu ya ushambuliaji akiwa na Daniel
Sturridge, amefunga jumla ya mabao 24 msimu huu kiasi kupelekea Rooney kuvutiwa na kiwango cha mshambuliaji huyu raia wa Uruguay.
Anakaririwa Rooney na MUTV akisema:
'Suarez, kwangu ni kwamba yuko juu kama walivyo akina Lionel Messi na Cristiano Ronaldo kama wachezaji bora duniani.
No comments:
Post a Comment