Mchakato wa ung’amuzi wa vipaji kwa ajili ya
maboresho ya Taifa Stars ulioshirikisha wang’amuzi wa vipaji (scouts) zaidi ya
40 umekamilika leo (Machi 15 mwaka huu) na majina ya wachezaji yatatangazwa
Jumatatu (Machi 17 mwaka huu)
Wachezaji hao watafanyiwa vipimo vya afya (medical
check up), kabla ya kuingia kambini Tukuyu mkoani Mbeya. Wachezaji watakaoingia
kambini ni wale watakaokuwa wamefaulu vipimo.
Wang’amuzi vipaji waliokuwa Lushoto ni Abdul
Mingange, Ayoub Nyenzi, Boniface Pawasa, Charles Mkwassa, Dan Korosso, Dk.
Mshindo Msolla, Edward Hiza, Elly Mzozo, Hafidh Badru, Hamimu Mawazo, John
Simkoko, Jonas Tiboroha, Juma Mgunda na Juma Mwambusi.
Kanali mstaafu Idd Kipingu, Kenny Mwaisabula, Kidao
Wilfred, Madaraka Bendera, Madaraka Selemani, Mbarouk Nyenga, Mohamed Ally,
Mussa Kissoky, Nicholas Mihayo, Pelegrinius Rutayuga, Peter Mhina, Salum
Mayanga, Salvatory Edward, Salum Madadi, Sebastian Nkoma, Sekilojo Chambua, Selemani
Jabir na Shabani Ramadhan.
Wengine ni Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF
ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ufundi, Kidao Wilfred, Mjumbe wa Kamati
ya Utendaji ya TFF ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Vijana, Ayoub Nyenzi,
Kaimu Mkurugenzi wa Ufundi, Salum Madadi na Mshauri wa Rais (Ufundi),
Pelegrinius Rutayuga.
No comments:
Post a Comment