Manchester City iliyobaki pungufu baada ya dakika kumi za kuanza mchezo dhidi ya Hull City baada ya mlinzi wake mahiri Vincent Kompany kutolewa nje kwa kadi nyekundu imefanikiwa kupata ushindi wa mabao 2-0 huku ikiendeleza presha kubwa kwa vinara wa ligi kuu nchini England Chelsea katika kilele cha msimamo wa ligi hiyo Barclays Premier League.
David
Silva alianza kuandika bao la kwanza baada ya mpira wa -superb long-range - dakika nne baada ya Kompany
kuonyeshwa kadi ya nyukundu ya moja kwa moja na mwamuzi Lee Mason kwa kumfanyia kitu mbaya Nikica Jelavic ambaye alikuwa akielekea langoni mwao.
Bao la pili la City limewekwa kimiani na Edin
Dzeko dakika ya mwisho ya mchezo.
No comments:
Post a Comment