Kikosi cha mabingwa wa soka Tanzania
Bara, Yanga kimepata msukosuko baada ya basi lao kutumbukia msingini katika eneo la
Mikese mkoani Morogoro.
Basi hilo limepata ajali takribani saa moja iliyopita wakati wakiwa njiani kurejea jijini Dar es Salaam baada ya mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Mtibwa Sugar kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini humo, jana.
Taarifa zinasema hakukua na majeruhi
lakini baadhi ya wachezaji walilazimika kujiokoa baada ya basi hilo kulikwepa
basi jingine ambalo lilikuwa linalifuata hilo la Yanga.
No comments:
Post a Comment