Aliyewahi kuwa
Mwenyekiti wa Simba, Hassan Dalali anayeaminika kuwa kiongozi anayependwa zaidi
na wanachama wa klabu hiyo katika kipindi hiki, jana alikutana na Mwenyekiti wa
sasa, Ismail Aden Rage na kupiga stori sana.
Rage aliomba kupiga picga na Dalali na kusema alichangia yeye kuingia kugombea uenyekiti wa Simba, lakini leo alitangaza kwa mara nyingine kwamba hatogombea tena nafasi hiyo katika uchaguzi wa Mei 4, mwaka huu.
Viongozi
hao wamekutana leo kwenye mkutano wa marekebisho ya katiba ya Simba
uliofanyika kwenye Ukumbi wa Maofisa wa Pilisi Oysterbay jijini Dar es
Salaam.
Pamoja na
hivyo, Rage alikumbatiana na aliyekuwa makamu mwenyekiti wakati wa uongozi
wake, Geofrey Nyange ‘Kaburu’ ambaye ilielezwa wamekuwa wapinzani kwa kipindi
sasa.
Rage na
Kaburu, ingawa wamekuwa hawaonyeshi, lakini wamekuwa hawaelewani kutokana na
mitazamo ya kimaendeleo, hali iliyochangia Kaburu kuamua kuachia ngazi kwa
manufaa ya klabu hiyo.
No comments:
Post a Comment