KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Monday, March 17, 2014

BONDIA FADHILI AWADH ALIYEFARIKI JANA KUZIKWA LEO MOROGORO

Bondia wa ngumi za kulipwa Fadhili Awadh amefariki dunia katika hospital ya Mwananyamala jijini Dar es Salaam baada ya kuugua kwa siku kadhaa. Fadhili Awadh alikuwa ni miongoni mwa mabondia waliochaguliwa kucheza  mpambano wa ubingwa tarehe 29 mwezi huu wa tatu dhidi ya mpinzani wake toka Tanga Alan Kamote, hivyo pia alikuwa katika maandalizi ya pambano hilo. Sababu ya kifo chake kwa ripoti ya daktari wa Mwananyamala ni kuwa Fadhili alikuwa na malaria na alitumia dozi ya metakafline kabla ya hali yake kubadilika alipojaribu kufanya  mazoezi na kujisikia vibaya na kuwahishwa katika hospitali hiyo ambayo alikaa kwa siku mbili akiendelea na matibabu na hatimae umauti ulipomkuta. Fadhili Awadh mwenye umri wa maika 32 alikuwa anaendelea vizuri katika mchezo huo kiasi cha kufikia kucheza pambano la ubingwa katika ukumbi wa PTA sabsaba, akiwasindikiza mabondia japhet kaseba na Thomas mashali . sisi tulimpenda lakini mungu alimpenda zaidi ,Ailaze roho ya marehemu Fadhili awadh “tiger” peponi,mwili wa marehemu umesafilishwa kwenda morogoro kwa ajili ya maziko bondia huyo enzi za uhai wake alicheza mapambano 12 amepoteza 5 na kushinda 7 ambapo mpambano wake wa kwanza katika harakati za ngumi za kulipwa alicheza tarehe
10/09/2010

No comments:

Post a Comment