
Mlinda mlango huyo mwenye umri wa miaka 17 tayari ameshaiwakilisha Serbia katika kikosi chake cha wachezaji wenye umri chini ya miaka 17 lakini atasalia katika klabu yake ya sasa ya FK Vojvodina kwa msimu wa 2014-15 akiendeleza kipaji chake.
United kwasasa ina walinda mlango watatu wazoefu katika kikosi chake ambapo Anders Lindegaard na Ben Amos wakiwa wanasubiri kwa David de Gea.
Kijana mwenye umri wa miaka 21 Sam Johnstone tayari amekamilisha mpango wa mkopo katika klabu ya Doncaster.
Red Devils wanatafuta namna ya kuboresha kikosi chao baada ya kumaliza katika nafasi ya saba msimu uliomalizika wa Premier League ambao aliyekuwa meneja wao David Moyes alipoteza kazi kufuatia kushindwa kutetea taji la ligi hiyo.
Kocha Mholanzi Louis van Gaal anajipanga kuchukua nafasi ya Moyes na imefahamika kuwa tayari Van Gaal ameanza kuingiza mipango yake mipya kwa matayarisho ya msimu ujao ambapo mlinzi wa Borussia Dortmund Mats Hummels na kiungo wa Roma Kevin Strootmat wakiwa katika orodha ya wachezaji wake anao wataka.
No comments:
Post a Comment