KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Monday, May 5, 2014

Mtaalamu wa FIFA akagua uwanja wa Kaitaba

Dr. Ian McClements akichimba chini ili kupima na kuona aina ya udongo ulio chini katika uwanja wa Kaitaba ulioko Bukoba kabla ya mradi wa uwekaji nyasi bandia kuanza.
 
Uwanja wa Kaitaba na Nyamagana jijini Mwanza vinatarajiwa kuwekwa nyasi bandia kwa ufadhili wa shirikisho la soka dunia FIFA chini ya mpango wa misaada wa Goal Projects. Baada ya ukaguzi huo, McClements atatuma ripoti yake FIFA ili shirikisho hilo liweze kuteua mkandarasi wa kufanya kazi hiyo.
Kwa Tanzania viwanja vilivyowekwa nyasi bandia hadi sasa kupitia Goal Project ni Uwanja wa Uhuru uliopo Dar es Salaam, Uwanja wa Karume (Dar es Salaam) na Uwanja wa Gombani uliopo Pemba.

No comments:

Post a Comment