KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Tuesday, November 30, 2010

MLINZI WA Liverpool Jamie Carragher kufanyiwa upasuaji wa begani na kukosekana mwezi mzima


Liverpool imethibtisha kuwa mlinzi wake Jamie Carragher kuwa atakuwa nje ya dimba kwa takribani miezi mitatu kufuatia kuelekea katika upasuaji wake wa bega.
Mlinzi huyo mwenye umri wa miaka 32 alipatwa na majeruhi katika mchezo wa ligi kuu ya kandanda nchini uingereza dhidi ya Tottenham,mchezo ambao livwerpool walikubali kichapo cha mabao 2-1huku shukurani kubwa zikipelekwa kwa Aaron Lennon akiifungia Spurs.
Mlinzi huyo anategemewa kuelekea kwenye upasuaji juma hili na matumaini ya kurejea kwake dimbani yatategemea na namna kasi ya kuponya jareha lake la upasuaji.
Maumivu ya Carragher yanakuwa pigo kwa liverpoool kufuatia Daniel Agger kuwa bado anaendelea kuponya majeraha yake huku Joe Cole na nahodha Steven Gerrard wote wakiwa bado wana sumbuliwa na msuli.

Arsene Wenger: Arsenal haitanunua mchezaji Januari


Meneja wa Arsenal Arsene Wenger amesisitiza kuwa hana nia ya kuongeza wala kupunguza mchezaji wake katika dirisha dogo la mwezi januari labda kutokee tatizo la majeruhi ndani ya kikosi chake
Timu hiyo toka pande za London ya kaskazini ilikuwa ikihusishwa na mpango wa kuvuta wachezaji kadhaa katika dirisha hilo la usajili hata hivyo taarifa hizo zimekanushwa na meneja huyo.
Akikaririwa anasema
"sera yangu ni kusalia na kikosi changu kama kilivyo hatutakuwa sokoni kwa namna yoyote.
"nataka kusalia na kikosi na nataka kuendelea na wachezaji hawa kwa hiyo hatutakuwa sokoni labda itokee kuwakosa baadhi yao kutokana na majeruhi"
Kumbuka Arsenal ipo katika nafasi ya tatu katika msimamo wa ligi kuu ya uingereza wakiwa wamezidiwa kwa points mbili na Manchester United walio katika nafasi ya pili.

Jose Mourinho akubali Real Madrid walikuwa nyuma kiubora dimbani hapo jana dhidi Barcelona

Kocha wa Real Madrid Jose Mourinho amekiri ya kuwa ni kweli kikosi chake hapo jana kilikuwa nyuma kiubora katika mchezo wa jana jana dhidi ya Barcelona katika mchezo wa ligi kuu ya kandanda nchini Hispania maarufu kama Elclasical.
Jose Mourinho amesema ilikuwa wazi kwa kupoterza kwa kichapo cha mabao 5-0 mbele ya Barcelona katika mchezo huo kwa kuwa kikosi chake maarufu kama Blancos hakikuwa bora dimbani kule Camp Nou.
Barca ilikuwa ikiongoza kwa mabao 2-0 mpaka mapumziko na hatimaye mpaka dakika tisini zinamalizika wakakubali kibano cha jumla ya mabao 5-0 na hivyo Real Madrid kushindwa kurejea katika uongozi wa ligi hiyo.
Barcelona sasa wanaongoza ligi hiyo ya Hispania wakiwa mbele kwa zaidi ya points mbili
Katika hatua nyingine nyota wa Madrid Xabi Alonso anasema si kwa kwamba kwa kupoteza mchezo wa jana usiku mbele ya Brcelona basi ndiyo matumaini yao ya kuwania taji la Hispania yameyeyuka
La Liga still has long way to go despite heavy defeat to Barcelona, says Real Madrid midfielder Xabi Alonso.
Mabao ya Xavi, Pedro Rodriguez, Jeffren, na mawili ya David Villa yalitosha kuwa nyong’onyesha Madrid na kuwa kipigo cha kwanza kikali kwa kocha msema hovyo Jose Mourinho ambaye jana alikuwa bubu ndani ya dakika tisini.
Alonso anasema baada ya mchezo ya mchezo walikaa na kufanya tathmini ya yale yaliyo tokezea na kusema mbele ya vyombo vya habari kuwa hatukutegemea mchezo kuwa namna ile kwa upande wetu lakini kuhusiana na kampeni za kuwania taji ligi bado kwani kuna michezo
Lakini wakati mchezo ukimalizika namna hiyo hesabu ya pasi ndani ya mchezo imeonyesha kuwa Barcelona walikamilisha pasi zaidi ya 600
Ndani ya pasi 684 zilizo chezwa na Barca asilimia 89% ya pasi zilifika eneo
Wakati hayo yakiwa hivyo kwa upande wa Madrid, walikamilisha asilimia 74% huku 224.94 zikifika mahala stahili.
ball possession mpaka dadika tisini ilikuwa ni Barca 67% na Mdrid 33%, huku jumla ya mashuti 15 yakielekezwa kunako lango la Real Madrid na wao Madrid wakipiga jumla ya mashuti 5.

No comments:

Post a Comment