Atletico Madrid yaendeleza rekodi ya kutokufungwa katika uwanja wake wa nyumbani |
Atletico Madrid imeendeleza rekodi yake ya kutokufungwa katika uwanja wake wa nyumbani katika ligi kuu ya Hispania La Liga mpaka sasa ikiwa imefikia michezo 24 baada ya kuibuka na ushindi wake mwingine hii leo dhidi ya Espanyol.
Tiago Mendes aliiandikia timu yake bao la uongozi kwa kichwa baada ya kupokea pasi ya Gabi Fernandez na kupiga kichwa mpira ulimshinda mlinda mlango Kiko Casilla.
Mabingwa hao walifanikiwakuongeza bao la pili katika kipindi cha pili kupitia kwa Mario Suarez aliyeupata mpira wa kichwa ulipigwa na Gimenez kutoka katika eneo la kona.
Ushindi huu una maana kuwa kikosi cha Diego Simeone kinasalia na nyuma kwa alama tano dhidi ya Barcelona lakini wakikamata nafasi ya nne katika msimamo wa ligi hiyo na wanaweza kusukumwa mpaka katika nafasi ya tano kama Sevilla watafanikiwa kuichapa Elche.
Atletico haijafungwa katika uwanja wake wa nyumbani katika ligi msimu huu tangu mara ya mwisho kufungwa na 2-1 na Barcelona May 12 2013.
Timu hiyo itakuwa tena uwanjani Vicente Calderon Jumatano watakapo wakaribisha Malmo ya Sweden katika mchezo wa ligi ya mabingwa Ulaya mchezo wa kundi A.
No comments:
Post a Comment