Huyu mama Portia Modise ameisaidia Afrika kusini kutinga nusu fainali ya fainali ya mataifa ya Afrika kwa wanawake huku yeye mwenyewe akiandika rekodi ya kuifungia nchi yake magoli 100 |
Afrika kusini imefanikiwa kusonga mbele katika hatua ya nusu fainali ya mataifa ya Afrika 2014 kwa wanawake baada ya kupata ushindi wa mabao 5-1 dhidi ya Algeria ambapo mshambuliaji nyota kabisa Portia
Modise akifunga magoli mawili na kupaisha rekodi yake ya ufungaji kufikia magoli 100 akiwa na timu ya taifa ya wanawake ya nchi hiyo.
Uwiano wa ushindi wa Banyana Banyana unamaanisha kuwa Ghana
imeshindwa kusonga mbele katika hatua hiyo ya nusu fainali licha ya ushindi wake waliopata wa bao 1-0 dhidi ya Cameroon ambaye tayati ilikwisha kufuzu kutoka katika kundi B.
Hilo ni pigo kwa timu ya Ghana wanawake maarufu kama 'Black Queens' ambao walikuwa na matumaini ya kutinga kwa mara nyingine tena katika fainali ya kombe la dunia Fifa kwa wanawake.
Kwa upande wake Portia Midise amekaririwa akisema
“Nililala jana na kuamka nikiwa na uhakika wa kufunga magoli mawili na nimefanya hivyo”
Afrika kusini itacheza na mshindi wa kundi A Nigeria katika nusu fainali huku mshindi wa kundi B Cameroon wakijipanga kukabiliana na Ivory Coast.
No comments:
Post a Comment