Pep Guardiola ameweka wazi kuwa baada ya Bayern Munich ataelekea England |
Pep
Guardiola huenda akaelekea kutoa huduma katika moja ya vilabu vya Premier League baada ya kutanabaisha wazi kabisa kuwa anategemea siku moja kuelekea nchini England.
Guardiola
yuko katika mkataba na Bayern Munich mpaka 2016 lakini anaonekana hana mpango wa kuendelea kuishi kwa muda mrefu na huenda akaendeleza kazi yake huko England.
Manchester
City inaonekana kupewa kipaumbele kumchukua Guardiola, ambako anaonekana kutaka kusogeza karibu urafiki wake na Txiki Begiristain, ambaye ni mchezaji mwenzake wa zamani katika kikosi cha Barca ambaye kwasasa ni mkurugenzi wa soka ndani ya kikosi cha City ambaye pia alikuwa akishikilia nafasi hiyo katika klabu ya Bareclona wakati Guadiola akiwa kocha.
Lakini wakati Pep Guardiola akiiangalia England hii itamfanya mtendaji mkuu wa klabu ya Arsenal Ivan
Gatzidis atakuwa katika hadhari kuona kama kama Wenger atasaini tena mkataba.
Wenger, mwenye umri wa miaka 65, alisaini mkataba wa miaka mitatu mwishoni mwa msimu lakini hitaji la mafanikio ilikuwa ni ajenda katika mkutano wa mwaka wa klabu hiyo wiki iliyopita
No comments:
Post a Comment