Hatimaye Arsenal imefanikisha kupata nafasi nyingine ya kumsainisha Thierry Henry mkataba wa kurejea katika klabu hiyo kwa mkataba wa miezi miwili.
Arsene Wenger alikuwa katika kigagaziko kwa muda kiasi cha kama amrejeshe mfungaji wake wa kihistoria katika klabu hiyo kukipa nguvu kikosi chake ili kumaliza ligi wakiwa katika moja ya nafasi nne za juu ya ligi ya nchini Uingereza.
Baada ya hayo sasa kutimia wamesikika wachezaji wa Arsenal wakisema
Welcome back: Alex Song na Robin van Persie wakimfuraia Thierry Henry
Ni kipindi ambacho kilikuwa kigumu kwa mzee wenger kufuatia Gervinho na Marouane Chamakh kuwa safarini barani Afrika katika fainali ya mataifa ya Afrika mwezi ujao
Robin van Persie anahitaji usaidizi katika sehemu ya ufungaji.
Wenger ameamua kutoa offer hiyo baada ya mshambuliaji huyo mwenye miaka 34 kurejea mapumziko nchini Mexico juma hili.
Henry ana mkataba wenye thamani ya dola za kimarekani milioni $4.5million sawa na pauni milioni £2.9m na klabu yake ya sasa ya New York Red Bulls lakini amekuwa katika mazoezi na klabu yake ya zamani Arsenal katika kipindi hiki ambapo MLS imemalizika na hatarejea nchini Marekani mpaka mwezi March.
Katika kipindi chote cha uwepo wake Arsenal ataitumikia jumla ya michezo saba ya ligi kuu pamoja na michezo ya FA Cup ukiwemo mchezo wa kwanza ligi ya mabingwa dhidi ya AC Milan hatua ya robo fainali.
Lakini hata hivyo msaada wake zaidi unahitajika katika Premier League ambako Wenger anahitaji msaada zaidi hususani katika michezo migumu dhidi ya Manchester United na Tottenham inayokuja.
Nahodha huyo wa zamani wa Arsenal aliifungia klabu jumla ya magoli 226 ambayo ni rekodi ya klabu hiyo kati ya miaka ya 1999 na 2007.
Kurejea kwake kunaamsha ari ya mashabiki wa klabu hiyo baaba ya kipindi cha kiangazi kuwapoteza akina Cesc Fabregas, Gael Clichy na Samir Nasri.
No comments:
Post a Comment