KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Thursday, December 15, 2011

Kipa mkongwe wa Ghana amepigwa chini

Kipa mkongwe wa Ghana amepigwa chini

Mlinda mlango mkongwe wa timu ya Taifa ya Ghana Richard Kingson ameachwa katika kikosi cha timu hiyo ambacho kinajipanga kwa ajili ya michuano ya mataifa ya Afrika mwezi ujao.

Taarifa zimesema kuwa kinda Adam Kwarasey ndiye mlinda mlango namba moja wa Black Stars.

Mcjhezaji mwingine aliyeingizwa kwa mara ya kwanza ni Jordan Ayew,ambaye atakuwa ni mtoto wa tatu wa nyota wa zamani wa Ghana Abedi Pele kuitumikia timu ya taifa ya Ghana katika fainali za mataifa ya Afrika.

Nyota mpiga mabao katika ligi kuu ya Ghana Emmanuel Baffour naye amejumuishwa katika kikosi hicho cha kocha Goran Stevanovic.

Kingson alikuwa ni chaguo la kwanza kwa Ghana katika fainali za mataifa ya Afrika mwaka jana pamoja na kombe la dunia lakini amekuwa hana timu ya kuchezea tangu alipoachwa na klabu yake ya Blackpool kufuatia kushuka daraja katika ligi kuu ya uingereza mwezi May.

Kwarasey amepata nafasi ya kuichezea Ghana akiwa anasukuma kandanda nchini Norway katika timu za vijana na sasa akichukua nafasi ya Kingson.

Mwingine anaelekea Equatorial Guinea na Gabon ni kiungo Charles Takyi,ambaye ni hivi karibuni amefanikiwa kubadili uraia zamani ilikuwa ikitajwa kuwa ana uraia wa ujerumani.

Ghana ni miongoni mwa timu zinazo pewa nafasi kubwa ya kutwa taji hilo wakiwa katika kundi la D pamoja na Botswana, Mali na Guinea na watakuwa katika mji wa Franceville kusini mashariki ya Gabon.

Dominic Adiyiah amechwa katika kikosi hicho licha ya kung’ara mwaka jana katika soka la Afrika na baadaye kuelekea nchini Uturuki katika klabu ya daraja la pili ya Karsiyaka.

Goalkeepers:

Adam Kwarasey, Daniel Adjei, Ernest Sowah

Defenders:

Samuel Inkoom, John Paintsil, Daniel Opare, Masahudu Alhassan, Lee Addy, John Boye, John Mensah, Jonathan Mensah, Isaac Vorsah

Midfielders:

Charles Takyi, Emmanuel Agyemang Badu, Derek Boateng, Anthony Annan, Mohammed Abu, Kwadwo Asamoah, Sulley Muntari, Andre 'Dede' Ayew

Strikers:

Emmanuel Baffour, Prince Tagoe, Derek Asamoah, Asamoah Gyan, Jordan Ayew

Angola na Cameroon waenda sare(1:1)

Angola usiku wa hapo jana ilishikwa na Cameroon na kulazimishwa sare ya bao 1-1 wakiwa nyumbani katika mchezo uliopigwa kaskazini mwa nchi ya Angola katika mji wa Cabinda.

Kocha wa Lito alikuwa akiuuchukulia mchezo kama sehemuya maandalizi ya kikosi chake kwa ajili ya michuano ya mataifa ta Afrika mwakani .

Cameroon iliwatumia zaidi wachezaji wanao cheza soka nyumbani na walikuwa katika kiwango kibovu katika dakika 21za mwanzo za mchezo pale ambapo Cabungula alipofunga bao kwa wenyeji .

Joseph alifanikiwa kupata bao la kusawazisha katika dakika ya 40th na hakukuwa na magolizaidi .

Angola sasa wanajipanga kukutana dhidi ya Zambia jumapili ya desemba 18th na siku nne baadaye watacheza dhidi ya Namibia.

Palancas Negras baadaye wataelekea nchini Brazil kwa ajili ya matayarisho yao ya mwishotarehe 6 January.

Michuano ya mataifa ya Afrika inatarajiwa kuanza kutimua vumbia January 21st mpaka February 12 katika nchi za Gabon na Equatorial Guinea na Amgola imepangwa katika kundi la B wakiwa na Burkina Faso, Ivory Coast na Sudan.

Mchezaji bora anayechezea soka ndani ya Afrika (African Player of the Year 2011 (Based in Africa)

(a) Oussama Darragi (Esperance Sportive de Tunis and Tunisia)

(b) Zouhir Dhaouadi (Club Africain and Tunisia)

(c) Banana Yaya (Esperance Sportive de Tunis and Cameroon)

Timu bora ya taifa (National Team of the Year)

(a) Botswana

(b) Cote d’Ivoire

(c) Niger

(d) Tunisia

Timu ya taifa bora ya wanawake (Women’s National Team of the Year)

(a) Cameroon

(b) Nigeria

(c) South Africa

Klabu bora ya mwaka (Club of the Year)

(a) Esperance Sportive de Tunis (Tunisia)

(b)Maghreb Association Sportive of Fez (Morocco)

(c) Wydad Athletic Club (Morocco)

Kipaji bora kilichochomoza (Most Promising Talent of the Year)

(a) Ahmed Elshenawy (El-Masry and Egypt)

(b) Souleymane Coulibaly (Tottenham Hotspurs and Cote d’Ivoire)

(c) Ahmed Musa (VVV Venlo and Nigeria)

Kocha bora wa mwaka (Coach of the Year)

(a) Harouna Doula (Niger)

(b) Nabil Maaloul (Esperance Sportive de Tunis) - Tunisia

(c) Stanley Tshosane (Botswana)

Mchezaji bora wa kike (Women’s Footballer of the Year)

(a) Nompumelelo Nyandani (South Africa)

(b) Perpetua Nkwocha (Nigeria)

(c) Miriam Paixao Silva (Equatorial Guinea)

Mwamuzi bora wa mwaka (Referee of the Year)

(a) Alioum Neant (Cameroon)

(b) Noumandiez Doue (Cote d’Ivoire)

(c) Djamel Haimoudi (Algeria)

Tuzo ya heshima kwa mkongwe- nguli (Legend Award)

Mustapha Hadji (Morocco)

Austin ‘Jay-Jay’ Okocha (Nigeria)

Yaya Toure guilty over Africa Cup of Nations departure

Kiungo wa Manchester City Yaya Toure anasema anajihisi kama mkosefu na kuchanganyikiwa kufuatia kuwa katika majukumu na timu yake ya taifa katika michuano ya mataifa ya Afrika mwezi ujao.

Toure anahitajika na taifa lake la Ivory Coast kwa ajili ya michuano hiyo inayotarajiwa kuanza kutimua vumbi katika nchi za Gabon na Equatorial Guinea January 12.

Anakaririwa akisema

"nchi yetu inatuhitaji mtu kama mimi na Drogba wakati huu ".

"kuna vita kwa mara nyingine na ni muhimu kufanya kitu kwa ajili ya watu wetu.ni hatari na watu wana hofu.

Mwaka mmoja baada ya vita vilivyotokana na uchaguzi wa urais ambao uliiweka Ivory Coast katika vita vya wenyewe kwa wenyewe ,vurugu na kuambatana na uchaguzi wa hivi karibuni umeleta hofu kubwa kama hali ilivyokuwa huko nyuma.

Licha ya kwamba hakuna vita vya wenyewe kwa wenyewe katika taifa hilo la Afrika magharibi , Toure anasema kuichezea timu ya taifa inaweza kutuliza zaidi hali ya mvutano ndani ya nchi yao.

"lazima niende kwasababu nchi yangu inapiatia katika hali ngumu ya vita.”.

Katika michuano ya mataifa ya Afrika Ivory Coast ipo katika kundi la B pamoja na mataifa ya Angola, Burkina Faso na Sudan

Katika hatua nyingine kiungo huyo wa Manchester City huenda akacheleweshwa kuondoka na klabu yake ili kwanza kutumika katika michezo miwili muhimu ya kuwania mataji.

City inataraji kukutana dhidi ya wapinzani wao wakubwa toka jiji moja la Manchester Man United mchezo wa michuano ya FA Cup mchezo wa mzunguko wa tatu na ambao utapigwa January 8, na mchezo mwingine ni dhidi ya Liverpool michuano ya Carling hatua ya nusu fainali siku tatu baadaye.

Lakini wakati hayo yakiwa hivyo ni kwamba Ivory Coast itakuwa katika na haki ya kuwa na wachezaji hao Toure na kaka yake Kolo kwa mujibu wa sheria za FIFA ambayo inasema timu shiriki inaweza kumuita mchezaji na kuripoti ndani ya siku 14 kabla ya kuanza michuano mikubwa.

Mwenyewe Yaya Toure ameonekana kutokuwa na wasiwasi juu ya kikosi cha Man City akisema kikosi chao ni imara kuweza kushirikiana hata kama yeye hatakuwepo .

Fernando Torres hauzwi-Villas-Boas

Meneja wa Chelsea Andre Villas-Boas amesisitiza kuwa mshambuliaji Fernando Torres hauzwi kwa gharama yoyote ile.

Villas-Boas amejibu mapendekezo yaliyotolewa kwamba Torres atauzwa katika kipindi cha dirisha dogo la usajili mwezi Januari kutokana na kutofanya vizuri mwaka huu katika viunga vya Stamford Bridge.

Villas-Boas Amesema si kweli na hapatikani kwa gharama yoyote.

"tuna uhakika wakati Fernando analetwa katika timu yetu ni kutokana na ubora na kipaji alichokuwanacho na tumefanya maamuzi bora kwa ajili ya timu.

Villas-Boas pia amejibu malalamiko ya hivi karibuni yaliyotolewa na kiungo mkongwe Frank Lampard kuhusu kuachwa katika kikosi cha kwanza.

Lampard alianzia benchi katika mchezo wa pili mfululizo dhidi ya Manchester City jumatatu lakini aliifungia goli la ushindi timu yake katika ushindiwa mabao 2-1 waliyoupata.

Akizungumzia hilo Boas amesema kuna wachezaji wengi ambao wanaweza kuwepo katika kikosi cha kwanza na Lampard hayupo peke yake.

Anadhani Lampard ni mmoja kati ya wachezaji bora watano ambao wamekuwa wakitumika zaidi na kila mchezaji anataka kujumuishwa katika kila mchezo lakini wakati mwingine si rahisi.

Berlusconi: Tevez can be Europe's best

Mmiliki wa AC Milan Silvio Berlusconi anaamini Carlos Tevez atashinda tuzo ya Ballon d'Or kama ataelekea San Siro na kumtaka mua-Argentina huyo kuamua kuaelekea Rossoneri kuliko Paris Saint Germain.

Tevez ambaye kwasasa anazidi kuongeza umri akiwa katika miaka 27, anataka kuondoka Manchester City na klabu hiyo inataka kumuuza mshambuliaji huyo lakini wakishindwa kufiakia maamuzi hayo kutokana bei stahili kutofikiwa huku klabu hiyo ikimuweka sokoni kwa euro milioni 35.

City ilishatupilia mbali offer moja ya Milan,ambao walikuwa wakimtaka Tevez kwa mkopo mpaka mwisho wa msimu kabla ya kusaini moja kwa moja kwa gharama ya euro milioni €25 million huku makamu wa Rais wa Rossoneri Adriano Gailliani hapo jana akisisitiza kuwa hawatakuwa na maongezi zaidi kwa mara nyingine zaidi ya kile kilicho tangazwa awali.

Wakati hayo yakiwa hivyo Berlusconi bado anaonekana kumuhitaji Tevez na kumsogeza katika ligi kuu ya italia “Serie A” na kusema kuwa nyota huyo atakuwa na na nafasi zaidi ya kung’ara huko Milan kuliko kuelekea PSG ambao nao wamekuwa wakihusishwa na kumtaka mshambuliaji huyo wa zamani wa Manchester United frontman lakini lakini wakiwa bado hawajaweka ile offer rasmi.

Berlusconi anasema

"kama anataka kushinda tuzo ya Ballon d'Or anatakiwa kuja huku ,'' na akaendelea kusema

"Tevez ana maamuzi moja kama anataka fahari na pesa.

"Milan ni kupata fahari na atakuwa na uwezekano wa kuonyesha kipaji dunaini kote na kushinda tuzo ya Ballon d'Or akiwa nasi . PSG wana nguvu ya pesa represents a strong economic force.lazima achague kati ya hayo mawili.''

Tayari Teves amearifiwa akitaka kurejea katika klabu yake ya zamani ya Boca Juniors.



No comments:

Post a Comment