Mabingwa wa soka Tanzania Bara Simba hii leo wamepuliza parapanda la kuanza kwa ligi kuu ya Tanzania bara kwa ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Azam fc katika mchezo wa ngao ya hisani uliopigwa katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Azam ndio waliokuwa wa kwanza kupata bao kupiti kwa John Boko na kabla ya bao pili kufungwa Kipre Tcheche kabla ya Simba kuandika bao lao la kwanza kwa njia ya penati kupiti kwa Daniel Akufor kufuatia ya Emmanuel Okwi kufanyiwa madhambi katika eneo la hatari.
Simba ilifanikiwa kuandika bao la kusawazisha kupitia kwa Emmanuel Okwi huku bao tatu likifungwa kwa shuti chini na kiungo maridhawa Mwinyi Kazimoto.
Kufanyika kwa mchezo huo kuna ashiria kuwa ligi kuu ya Tanzania bara kuanza ambayo imepangwa kuanza jumamosi hii.
No comments:
Post a Comment