KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Friday, November 9, 2012

KOCHA MILOVAN WA SIMBA KUWAKOSA KASEJA NA AMIRI MAFTAHA MCHEZO WA KESHO DHIDI YA TOTO AFRIKANS

 Wakati Simba kesho inajipanga kumaliza duru la kwanza la ligi kuu ya soka Tanzania Bara dhidi ya Toto Afrikans mchezo ambao umepangwa kufanyika katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, wachezaji wawili muhimu wa timu hiyo Juma Kaseja na Amir Maftaha wenyewe hawatakuwepo katika orodha ya wachezaji wawakilishi katika kikosi cha timu hiyo.

Akiongea hii leo katika makao makuu ya klabu hiyo afisa habari wa klabu hiyo Ezekiel Kamwaga amesema kocha Milovan Circovich atamkosa mlinzi wake wa kushoto Amir Maftaha ambaye amefanyiwa upasuaji mdogo wa uvimbe ulikuwepo kichwani upasuaji ambao umefanyika jana.

Pia Milovan atakosa huduma ya mlinda mlango namba moja wa klabu hiyo Juma Kaseja ambaye imearifiwa kuwa ameomba ruhusa ya kupumzika katika kipindi hiki.

Kamwaga amesema kuwa Kaseja ameomba  kupumzika kutokana na tuhuma nzito za kuhujumu timu zilizo elekezwa kwake baada ya mchezo dhidi ya Mtibwa uliofanyika mwishoni mwa juma lililopota ambapo mabingwa hao watetezi wa taji walifungwa mabao 2-0.

Kwa mantiki hiyo ni dhahiri shahiri kuwa mlinda mlango wa kesho atakuwa ni kati ya William Mweta au Hamadi Waziri Mwinyimani.
 
 Simba inaingia dimbani katika mchezo wa kesho ikiwa inahitaji ushindi na alama tatu muhimu ambazo zitawasogeza mpaka kufikia alama 26 ambazo ni sawa na za mtani wake Yanga anayeongoza ligi hiyo.

Endapo Simba itashinda mchezo huo basi watakuwa wamerejea kileleni katika msimamo wa ligi angalau kwa siku moja wakisubiri matokeo ya mchezo wa jumapili kati ya Yanga na Coast Union mchezo ambao utachezwa mkoani Tanga katika dimba la Mkwakwani.