Xavi Henandez amesema
klabu yake ya Barcelona ya kichapo cha mabao 2-1toka kwa Celtic na sasa
kuangalia mchezo wao ujao dhidi ya Spartak Moscow bila kujali matokeo
yakushangaza yaliyopita.
Barcelona
ilikamuliwa na mabingwa hao wa uskochi Celtic katika dimba la Celtic Park wa
jana jumatano ambapo kiungo huyo wa kimataifa wa Hispania anaamini kuwa
wanapaswa sasa kuondoa vichwani mwao kichapo hicho na kuangalia mbele safari
yao ya Urusi kuwafuata Spartak Moscow Novemba 20.
“mchezo
muhimu sasa ni kule Moscow, tunapaswa kuwa katika uongozi wa kundi ”
“tumekosa
nafasi hiyo dhidi ya Celtic, sasa itategemea na sisi wenyewe. Tunapaswa
kuelekea huko kusaka ushindi ukiwa ni mmoja wa michezo yetu miwili iliyosalia”
Baada ya mchezo
dhidi ya Spartak, kikosi cha kocha Tito Vilanova kitarudi nyumbani kucheza
dhidi ya Benfica Camp Nou hiyo itakuwa Desemba 5.
Licha ya
kufunga hiyo jana bado Barcelona imeendelea kukalia usukani wa kundi G wakiwa
na alama tisa alama mbili zaidi ya Celtic, alama tano zaidi ya Benfica na alama
sita zaidi ya Spartak.
Sergio Ramos anasema anacheza mpira akiwa katika maumuvu makali kwa kuwa wachezaji wengi ni majeruhi.
Mlinzi wa Real
Madrid Sergio Ramos amesema amekuwa akikabiwa na maumivu lakini amekuwa
akicheza kwa kuzuia maumivu kusaidia kikosi cha timu yake ambayo imekosa mlinzi
aliye ambaye yuko fiti.
Wenzake
walinzi wa pembeni Marcelo na Fabio Coentrao bado wanaendelea kusumbuliwa na
majeraha wakati huu ambapo Alvaro Arbeloa pekee ndiye aliyerejea baada ya kuwa
nje ya uwanja kwa muda sasa.
Ramos amesisitiza
kuwa ameamua kucheza licha ya kuwa na maumivu ya misuli kwakuwa asingependa
kuwaangusha wenzake.
"ni
kweli siko katika hali nzuri kwa asilimia 100 na hii ni kutokana na maumivu ya
misuli, huu si wakati wa kuacha kucheza kwasababu tuna wachezaji wengi muhimu
majeruhi katika eneo la ulinzi. Tunapaswa kuwepo pale kama timu"
Ramos mwenye
umrik wa miaka 26 ametoa huduma mara 15 katika kikosi cha Madrid tangu kuanza
kwa msimu huu.
Ibrahimovic amesimamishwa michezo
miwili ya Ligue 1
Zlatan Ibrahimovic
amesimamishwa kucheza michezo miwili kufuatia kutolewa nje ya uwanja katika
mchezo baina ya Paris Saint-Germain dhidi ya Saint Etienne mchezo ambao
walifungwa mabao 2-1 jumamosi iliyopita.
Mshambuliaji
huyo mwenye umri wa miaka 31 alionyeshwa kadi nyekundu ya moja kwa moja
iliyotokana na kumchezea vibaya mlinda mlango Stephane Ruffier baada ya
kunyanyua daruga kifuani kwake katika harakati za kuwania mpira.
Mwenyekiti
wa LFP Pascal Garibian amesema adhabu hiyo imechukuliwa kama mgongano baina ya
wachezaji hao ulikuwa kama ajili.
"Ibrahimovic
amesimama kwa michezo miwili kwa kucheza rafu mbaya ambayo imehatarisha hali ya
mchezaji mwenzake "
Ibrahimovic atakosekana
katika mchezo dhidi ya mabingwa wa taji la ‘League 1’ Montpellier jumamosi hii
pamoja na mchezo dhidi ya Rennes Nov. 17.
Ibrahimovic amefunga
jumla ya mabao 10 katika Ligue 1 msimu huu na kukisaidia kikosi cha kocha Carlo
Ancelotti kukalia usukuani wa ligi ya nchini Ufaransa wakiwa na alama 22 baada
ya michezo 11.
Wilshere, Sterling, Shelvey &
Osman watajwa kikosi cha England
Kiungo wa Arsenal
Jack Wilshere ameitwa tena kuunda kikosi cha timu ya taifa ya soka ya England tayari
kwa mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya Sweden.
Wilshere
mwenye umri wa miaka 20 amerejeshwa kikosini baada ya kuwa majeruhi kwa zaidi
ya mwaka mmoja ambapo aliitumikia England mchezo mmoja.
Wapo
wachezaji ambao wameitwa kwa mara ya kwanza ikiwa ni pamoja na kiungo wa Everton
Leon Osman, Raheem Sterling wa Liverpool na kinda Jonjo Shelvey.
Nahodha wa
Liverpool Steven Gerrard yupo kikosini kwa mara nyingine tena na anatarajiwa
kuwa mchezaji wa sita wa England kutimiza michezo 100 ya kuitumikia timu ya
taifa.
Wachezaji
wengine ambao huko nyuma waliwahi kuichezea timu ya taifa kwa zaidi ya michezo
100 ni pamoja na Peter Shilton aliyechezea michezo 125,David Beckham michezo 115,
Bobby Moore michezo 108, Bobby Charlton michezo 106 na Billy Wright jumla ya
michezo 105.
Kikosi cha
sasa kinabadiliko ya wachezaji 10 tofauti na kile kilichocheza mchezo wa kuwania
kufuzu kombe la dunia dhidi ya Ukraine na Poland.
Ashley Cole
ambaye ameshaitumikia England jumla ya michezo 99 ameachwa kutokana na
kutokuwepo katika kikosi cha Chelsea kulichokuwepo dimbani katika mchezo dhidi
ya Shakhtar Donetsk hapo jana akisumbuliwa na maumivu ya msuli.
Joleon
Lescott, Adam Johnson, James Milner, Andy Carroll, Kieran Gibbs, Michael
Carrick, Frank Lampard, Alex Oxlade-Chamberlain na Jermain Defoe wote
hawatakuwepo katika mchezo huo utakaopigwa mjini Stockholm.
Goalkeepers:
Fraser Forster (Celtic), Joe Hart (Manchester City), John Ruddy (Norwich City).
Defenders:
Leighton Baines (Everton), Ryan Bertrand (Chelsea), Gary Cahill (Chelsea),
Steven Caulker (Tottenham), Phil Jagielka (Everton), Glen Johnson (Liverpool),
Ryan Shawcross (Stoke City), Kyle Walker (Tottenham).
Midfielders:
Tom Cleverley (Manchester United), Steven Gerrard (Liverpool), Aaron Lennon
(Tottenham), Leon Osman (Everton), Jonjo Shelvey (Liverpool), Raheem Sterling
(Liverpool), Theo Walcott (Arsenal), Jack Wilshere (Arsenal), Ashley Young
(Manchester United).
Forwards:
Wayne Rooney (Manchester United), Daniel Sturridge (Chelsea), Daniel Welbeck
(Manchester United).
No comments:
Post a Comment