Mama
wa Mitindo nchini Tanzania, Asia Idarous kupitia Kampuni yake ya Fabak
Fashions wanakuletea onyesho kubwa la Khanga za Kale litakalofanyika
Novemba 23, 2012 katika Hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam.
Onyesho hili kubwa ambalo limekuwa
likifanya vizuri kwa takribani miaka minne sasa na kupata mafanikio
makubwa ndani na nje ya Tanzania hasa katika nchi ya Marekani,
litawakutanisha wabunifu zaidi ya 30 kutoka sehemu mbali mbali ambao nao
wataonyesha mavazi yao waliyoyabuni.
Watu Maarufu hapa nchini watapanda
jukwaani siku hiyo kuonyesha Mavazi ya Khanga za Kale kutoka kwa Mama
wa Mitindo, Asia Idarous Khamsin ambapo fedha itakayopatikana kutokana
na onyesho hilo itapelekwa kwenye Kituo cha Kulea watu walioathirika na
Madawa ya Kulevwa kilichopo Kikale Wilayani Rufiji, Mkoani Pwani kwa
ajili ya kumalizia ujenzi.
No comments:
Post a Comment