Meneja wa Arsene Wenger wa Arsenal amemjia juu mwamuzi Chris Foy kwa kumtoa nje ya uwanja Mikel Arteta
katika mchezo wao wa leo dhidi ya Crystal Palace, akisisitiza kuwa alifanya maamuzi ya uongo.
Arteta alitolewa nje ya uwanja kwa kadi nyekundu ya moja kwa moja baada ya kumfanyia madhambi mshambuliaji wa zamani wa klabu hiyo Maroune Chamakh wakati akikaribia lango la washika mitutu.
Wenger amesema maamuzi ya Foy ya kumtoa nje Arteta yalikuwa si sahihi.
‘Arteta hakuwa mtu wa mwisho na ilikuwa ni fursa ya mshambuliaji kufunga. Chamakh alikuwa mbali na goli na faulo ilikuwepo ndiyo.’
No comments:
Post a Comment