Mikel Arteta na Olivier Giroud hii leo wameisaidia timu yao ya Arsenal iliyokuwa na wachezaji 10 uwanjani kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Crystal Palace isiyo na meneja, na hivyo klabu hiyo kufanikiwa kuendeleza na kuimarisha uongozi wao wa ligi ya Premier.
Penati ya kipindi cha pili iliyopigwa na Mikel Arteta iliwapa bao la kwanza licha ya kuwa baadaye Arteta alizawadiwa kadi nyekundu na kutolewa uwanjani kabla ya Olivier Giroud kuimarisha ushindi huo kwa kuandika bao la pili la kichwa.
Ilikuwa ni tofauti kidogo licha ya kichapo hicho kwa Palace kwani walionekana kuichachafya Arsenal na hata kupata nafasi kadhaa katika mchezo huo uliopigwa Selhurst
Park.
Arsene Wenger ambao leo alimpumzisha Jack Wilshere, na kumpoteza Mathieu Flamini
mapema pia waliwanyima nafasi Palace ambao pengine wangetumia mapungufu makosa ya mlinda mlango Wojciech Szczesny.
Wenyeji walipigana mpaka mapumziko ambapo walikwenda suluhu lakini nguvu kubwa waliyotumia sekunde 90 za kipindi cha pili ziliwagharimu pale Adlene Guedioura alipomfanyia madhambi Serge Gnabry ndani ya kisanduku cha hatari.
Arteta aliandika bao kabla ya kutolewa kwa kumfanyia madhambi mshambuliaji wa zamani wa klabu hiyo Maroune Chamakh.
No comments:
Post a Comment