Moshi: Bomu la kurusha kwa mkono la moshi lililorushwa baada ya bao kuingia
Bomu likiondolewa uwanjani
Huduma ya kwanza
Mabomu ya moshi yamerejea tena katika soka ikiwa ni siku sita tu zimepita baada ya mwamuzi msaidi David Bryan kupigwa na kitu mgongoni na mashabiki.
Msahabiki wa Barnsley walitupa bomu la moshi wakati wakiwa nyuma kimatokeo kwa bao 1-0 katika mchezo wa watani wa soka wa eneo moja huko Yorkshire maarufu kama (Yorkshire derby) dhidi ya Sheffield Wednesday.
Shabiki mmoja alilazimika kusindizwa kutoka jukwaani kwa ajili ya kupewa matibabu.
Itakumbukwa kuwa watu wawili wenye umri wa miaka 25 na 47, walitiwa nguvuni na jeshi la polisi na kufunguliwa mashitaka baada ya tukio lingine kutokea katika uwanja wa Villa Park, kufuatia mwamuzi msaidizi Dave Bryan kutupiwa bomu la moshi shingoni kwa nyuma wakati mashabiki wa Tottenham walipokuwa wakishangilia goli la kwanza.
Wawili hao wamezuiliwa kuhudhuria mechi mpaka mahakama itakapo sikiliza kesi dhidi yao Novemba 28.
FA pia inachunguza tukio hilo ambapo imetoa taarifa yao ambayo ililaani viterndo hivyo na pia kujihukumu kwa kutokuwa makini watu kuingia na vitu vya hatari viwanjani.
Naibu konstable mkuu Andy Holt, ameweka wazi kuwa ni tatizo linalo ongezeka.
Likiwa hewani kabla ya kutua: Watu wawili wanashikiliwa baada kumtupia mwamuzi msaidizi David Bryan bomu mgongoni angalia picha bomu likotoka kwa mashabiki wa Tottenham iliyopita.
Amenukuliwa akisema
'Mwaka jana tulishihudia kuongezeaka kwa urushwaji wa miale na vitu vya moshi kwa asilimi 140 zaidi ya msimu uliotangulia ,'
'Kukamatwa kwa watuhumiwa kulikuwa kwa asilimia 150 bila shaka ni matukio ambayo yanonekana kukua inatutisha kwakweli'.
Investigation: Both the Polish and English FA's are being investigated after fans brought flares into Wembley
Arrests: 16 Polish fans were arrested at the match
Mashitaka yamefunguliwa na shirikisho la soka duniani FIFA dhidi ya FA kufuatia tukio lingine la uwanja wa Wembley wakati wa mchezo wa kuwani kufuzu kombe la dunia baina ya England na Poland Oktoba 15.
Chama cha soka cha Poland (Polish FA) pia kinachunguzwa baada ya taarifa ya waamuzi wa mchezo huo kupokelewa na kuelezea juu ya hilo kwa bodi ya uongozi ya FIFA.
Metropolitan Police iliwatia mikononi mashabiki 16 wa Poland kwa kurusha miale ya moto uwanjani lakini kesi ikawaangukia waendeshaji wa uwanja huo.
The English FA are being investigated for allowing the flares into the stadium
FIFA haijasema uchunguzi huo utachukua muda gani na ni adhabu gani itakayotolewa.
No comments:
Post a Comment