KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Friday, October 25, 2013

MASUMBWI: MWINGEREZA CHISORA KUKUMBANA NA KISIKI CHA ITALIA MODUGNO NOVEMBA 30.

Dereck Chisora anataka kufanya kazi kubwa mwezi ujao pale atakapo kuwa na kazi ya kutetea taji lake la Ulaya la uzito wa juu dhidi ya bondia asiyepigika Matteo Modugno.

Chisora toka katika jiji la London alishinda mapigano yote matatu mwaka huu na anamatarajio ya kuongeza taji lingine kwa kumchapa Modugno na kumjumuisha katika orodha ya vibonde wake.
Chisora alishinda taji la Ulaya baada ya kumchapa Mjerumani Edmund Gerber ndani ya raundi tano na sasa anataka kuendeleza ubabe wake dhidi ya mpinzani wake mrefu wa futi sita kutoka Langhirano Italia, ambaye naye anarekodi nzuri ya ushindi mfululizo katika mapambano 14.
Modugno ni bingwa wa Italia ambaye katika mapambano yake manne ya mwisho alishinda kwa KO ambapo pia bondia huyo mwenye umri wa miaka 26 aliwahi kumchapa mwenzio kutoka nchini Italia na bingwa wa Ulaya Paolo Vidoz.
Fired-up Chisora hatasubiri kukabiliana na Modugno na kumchapa katika mchezo ambao utapigwa Copper Box Arena ndani ya Olympic Park jijini London Jumamosi ya Novemba 30.

‘Modugno won’t be going the distance with me he’s getting smashed early,’ said Chisora.

No comments:

Post a Comment