Afrika kusini itakutana dhidi ya mabingwa wa Ulaya na dunia Hispania katika mchezo wa kimataifa wa kirafiki mchezo ambao umepangwa kufanyika jijini Johannesburg Novemba 19.
Rais wa chama cha soka nchini Afrika kusini (Safa), Dr Danny Jordaan, amesema mchezo utakuwa ni mwanzo wa Bafana bafana kucheza na vigogo vingine.
Aamekaririwa akisema Jordan
"Ni ndoto yetu imekuwa kweli hususani kwa mashabiki ambapo kwa mara nyingine watawaona wakali kama akina Iniesta na Xavi wakiwa uwanjani,".
Shirikisho la soka nchini Hispania limesema limefurahishwa kurejea katika jiji hilo na uwanja ambao walishinda kombe la dunia mwaka 2010 kupitia bao la Andres Iniesta.
No comments:
Post a Comment