KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Thursday, January 24, 2013

AKIWA MAKAO MAKUU YA FIFA RAIS KIKWETE AMESEMA HAYA.

Kikwete: Football can contribute to peace
Rais Jakaya Kikwete wa Tanzania ametembelea makao makuu ya shirikisho la soka duniani FIFA hapo jana ambapo alikutana na kufanya mazungumzo na Rais wa shirikisho hilo Joseph Sepp Blatter.
Amenukuliwa akisema. “Namshukuru Rais President Blatter kwa mwaliko wake wa heshima hapa makao makuu ya FIFA nyumbani kwa mchezo ambao wote tunaupenda"
 "Nampongeza pia Rais Blatter kwa kazi kubwa ya kuendeleza soka tangu aingie katika kazi yake, mchezo huu umeleta maendeleo makubwa na kupiga hatua kubwa."
"Pia nakubalina na nia yake Rais Blatter aliyoionyesha ya kuendeleza soka barani Afrika ni kutokana na juhudi zake ndio maana leo Afrika inaingiza timu tano katika fainali za kombe la dunia kama ilivyokuwa fainali zilizo pita 2010 katika ardhi ya Afrika.
Rais Kikwete amesema Tanzania imekuwa ikipokea misaada mingi kutoka FIFA kwa miaka mingi, na anatarajia hilo litaendelezwa mpaka vijana wa Kitanzania wote wakiume na wa kike watakapo kuwa wameingia katika mchezo huo.
 
Amesema kwa bahati mbaya kwasasa Tanzania inapigana kuhakikisha inafika katika kiwango cha juu cha soka la dunia lakini uvumilivu unahitajika na mafanikio yatakuja na anaamini katika hilo.
 
Rais Kikwete ambaye ni mchezaji wa zamani wa mchezo wa Kikwete pia ni mpenzi mkubwa wa soka mchezo ambao unapendwa na watu wengu duniani.

Amekaririwa akisema 
“Nimecheza mpira wa kikapu na soka , lakini nilipenda sana kikapu mchezo ambao kwa kiasi fulani nilionyesha kipaji changu, ndio maana niliambiwa nijitume zaidi katika mchezo huo kuliko soka ambao niliwaacha wenzangu wazuri katika mchezo huo waendelee, nadhani nilifanya uchaguzi sahihi”

Tukirudi nyuma katika suala la ulinzi wa amani barani Afrika hususani katika ukanda wa maziwa makuu hususani Burundi na Congo DR, Rais Kikwete akiwa huku amesema anaamini soka ina nguvu kubwa ya kuleta amani na kuwaleta watu pamoja.
 
Amenukuliwa akisema 
 "Soka inaeweza kutoa mchango mkubwa katika suala la amani"
 Amesema
 "Hata kama nchi iko katika vita watu wanacheza soka hata kwa mataifa ambayo yako katika hali ya kiurafiki kisiasa au kidiplomasia, mara nyingi wanajikuta wakicheza katika dimba la soka, na hakuna matatizo."Hiyo ni kauli ya Rais Kikwete huko FIFA.

No comments:

Post a Comment