Wakati
mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kuwania ubingwa wa
Tanzania Bara unaanza Jumamosi (Januari 22 mwaka huu), mzunguko wa pili
wa Ligi Daraja la Kwanza (FDL) umesogezwa mbele kwa wiki moja ambapo
sasa utaanza Februari 2 mwaka huu.
Uamuzi
wa VPL kuendelea Januari 26 mwaka huu ulifikiwa katika kikao cha Kamati
ya Ligi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na klabu za ligi
hiyo kilichofanyika jana (Januari 21 mwaka huu) jijini Dar es Salaam.
Hata
hivyo, uamuzi huo umefikiwa huku yakiwepo masharti kadhaa kutokana na
uamuzi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kukamata sh. milioni 157
kwenye akaunti za TFF, fedha ambazo zilitoka kwa mdhamini wa VPL
(Kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom) kwa ajili ya timu zinazoshiriki
ligi hiyo.
Masharti
hayo yatawasilishwa na Kamati ya Ligi kwa maandishi kwa Katibu Mkuu wa
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), nakala kwa Waziri wa
Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo. Awali klabu kupitia Kamati ya Ligi
zilisisitiza zisingecheza ligi hadi fedha hizo zitakaporejeshwa.
Kwa
upande wa FDL itaanza bila timu ya Small Kids ya Rukwa ambayo
imeshushwa daraja kwa mujibu wa kanuni baada ya kushindwa kucheza mechi
mbili katika mzunguko wa kwanza.
Kwa mujibu wa kanuni za ligi hiyo, matokeo yote ya mechi ambazo Small Kids ilicheza katika mzunguko huo wa kwanza yamefutwa. (Ratiba ya VPL imeambatanishwa).
No comments:
Post a Comment