Mzunguko wa
pili ya Ligi Kuu ya Vodacom utaanza Januari 26 mwaka huu huku kukiwa na maombi
ya televisheni ya SuperSport kuonesha mechi za Super Week kama ilivyokuwa
katika mzunguko wa kwanza.
Raundi tano
za awali katika ratiba ya mzunguko wa pili zinabaki kama zilivyo wakati
nyingine zilizobaki zitatolewa baada ya kuingiza mechi za Super Week.
Wakati huo
huo, mzunguko wa pili wa Ligi Daraja la Kwanza unatarajia kuanza Januari 26
mwaka huu. Ratiba ya ligi hiyo na tarehe rasmi ya kuanza itatangazwa baada ya
kupitiwa na Kamati ya Ligi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
inayotarajiwa kukutana mwishoni mwa wiki.
No comments:
Post a Comment