KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Saturday, February 2, 2013

KIMATAIFA:Anzhi Makhachkala yamsajili Mbrazil William. Balotelli anasema hakuna cha kukosa baada ya kuondoka England zaidi ya uzuri wa ligi kuliko zote ulaya na West Brom yamvuruga Odemwingie.



Anzhi Makhachkala wamethibitisha kumsajili kiungo wa Brazil WillianBorges da Silva kutoka klabu ya Shakhtar Donetsk kwa ada ya uhamisho ya euro milioni €35.



Willian mwenye umri wa miaka 24 hapo kabla alikuwa akihusishwa na vilabu viwili vya Chelsea na Tottenham lakini imethibitika kuwa sasa amejiunga na klabu hiyo inayoshiriki ligi kuu ya nchini Russia kwa mpango wa muda mrefu zikiwa ni taarifa zilizo andikwa katika mtandao wa klabu hiyo hapo jana.

Anzhi ilikuwa katika jitihada za mwisho usiku wa alhamisi na imekamilisha uhamisho huo wa thamani katika dirisha la mwezi Januari.
Taarifa ya mtandao wa Shakhtar imesomeka:
“FC Shakhtar na FC Anzhi wamefikia makubaliano juu ya uhamisho wa Willian kuelekaa katika klabu hiyo ya nchini Russia kwa thamani ya euro milioni 35.
“Shakhtar inamshukuru Willian kwa utumishi wake ndani ya klabu hiyo, akifunga magoli na kuonyesha uweledi wake. Tunamtakia kila la kheri katika timu yake mpya”
Tangu ajiunge na Shakhtar akitokea Corinthians mwaka 2007, Willian ameichezea michezo 221 na kufunga jumla ya magoli 37.
Anatarajiwa kujiunga na kambi ya timu yake mpya iliyoko Marbella hii leo. Atakuwa akijiunga na wachezaji kadhaa wa kibrazil pamoja na wakali kadhaa kama Samuel Eto'o na Lassana Diarra.
 
Balotelli: Hakuna cha kukumbuka England
 Mario Balotelli amewashukuru mashabiki wa Manchester City kwa kumuunga mkono lakini mshambuliaji huyo wa AC Milan amesema hakutakuwa na kitu cha kumfanya ajione anakikosa kwa kwa kuondoka England.
Mario Balotelli anamatumaini makubwa ya kuwepo kwa muda katika klabu yake mpya ya AC Milan
Balotelli mwenye umri wa miaka 22, amerejea Italia baada ya kuwa na nafasi finyu katika klabu yake ya zamani ya Manchester City ambako alikuwa katika vita kubwa ya kuwania namba na wakali wengine kama Sergio Aguero, Carlos Tevez na Edin Dzeko.
Akiongea katika mkutano wa utambulisho wake kwa waandishi wa habari  kama mchezaji wa Milan, mchezaji huyo alikosoa mambi mengi yanayo husu utamaduni wa kingereza lakini pia hakusita kuonyesha kusikitishwa kwake kwa kuiacha ligi ya England ‘Premier League’.
Amenukuliwa akisema
"Niseme ahsante kwa mashabiki wa City kwasababu wamekuwa wakarimu kwangu na wamekuwa wakinipa sapoti  vyote vya shida na raha”
 "Na niwashukuru wachezaji wenzangu na meneja pia, kingine ni kwamna ninafuraha nimeondoka England.
"Kwa dhati kabisa niseme ‘Premier League’ ni ligi nzuri sana na nadhani ndio ligi bora, Kwa mashabiki na uwanjani  ... it's an amazing league. Si kama katika siku za usoni nitarejea huko, kwasasa niko hapa"

Odemwingie: West Brom imenivuruga
 Peter Odemwingie ameinyooshea kidole klabu yake ya West Bromwich Albion kwa kushindwa kufanikisha uhamisho wake wa kuelekea Queens Park Rangers.
Odemwingie amepewa mapumziko ya siku chache baada ya kuondolewa akiwa mazoezini hapo jana.
Alikuwa kwenye mpango wa uhamisho wa mwezi januari ambapo alhamisi alielekea maskani ya QPR iliyoko Loftus Road huku nyuma taarifa ya West Brom ikitoka ambayo ilisema mchezaji huyo hakuwa na ruhusa na kuongea na QPR licha kuelekea huko.
Dirisha la usajili wa mwezi Januari limefungwa huku Odemwingie akishindwa kukamilisha mipango yake yha uhamisho ambapo jana alirejea kufanya mazoezi na klabu yake West Brom ambapo kulitokea kutokuelewana kabla ya kuondolewa mazoezini na kupewa mapumziko ya siku chache.

Taarifa zinasema hapo kabla West Brom ilikuwa katika hali ya kuwa tayari kumruhusu kuondoka, lakini baada ya kukosa mchezaji mbadala yake ndipo walipo amua kwa makusudi kusitisha mpango huo.

No comments:

Post a Comment