KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Wednesday, February 20, 2013

LIGI KUU TANZANIA BARA: SIMBA YAREKEBISHA MAKOSA NAYO AZAM YAIKAMATA TENA YANGA KILELENI.

Ligi kuu ya soka Tanzania Bara imeeleendea tena hii leo kwa michezo minne kuchezwa katika viwanja vinne tofauti.

Kule katika uwanja wa kumbukumbu ya Sokoine mjini Mbeya mabingwa watetezi wa taji Simba walikuwa wakikumbana na maafande wa jeshi la magereza Tanzania Prisons mchezo ambao umemalizika kwa Simba kuibuka na ushindi wa bao 1-0 lililofungwa na kiungo Amri Kiemba.

Matokeo ya mchezo huo yanaifanya Simba ifikishe jumla ya alama 31 hivyo kuibua matumaini ya kuendelea kulitetea taji lake, kufuatia kupata sare mfululizo kabla ya mchezo wa leo.

Katika uwanja wa Azam Complex kule Mbande nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam wenyeji Azam fc ambao ni wawakilishi wa Tanzania katika michuano ya kombe la shirikisho walikuwa wenyeji wa JKT Ruvu ambapo wamefanikiwa kuichapa kwa mabao 4-0.
Mabao ya Azam yamefungwa na Hamisi Mcha, John Bocco na Abdi Kassim.
Azam kwa mara nyingine ineendelea kuikaba koo Yanga katika usukani wa msimamo wa ligi wakiwa wote wana alama sawa 36.
 
Matokeo ya kushangaza ni katika uwanja wa CCM Kirumba Mwanza ambapo wenyeji Toto Afrikas walikuwa wakicheza dhidi ya Afrika lyon ya jijini Dar es Salaam ambapo Lyon imefanikiwa kupata ushindi wake wa tatu tangu kuanza kwa ligi kuu msimu huu baada ya kuifunga Toto nyumbani kwa mabao 2-0.
Katika uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga wenyeji Coast Union ya huko ilikuwa dimbani dhidi ya JKT Oljoro ya Arusha ambapo dakika 90 za mchezo zimeshuhudia Coast wakiibuka na ushindi wa mabao 2-0 mabao hayo yakifungwa Selemani Kassim Selembe na Jerry Santo.
Kwa matokeo hayo ni kwamba Coast sasa imefikisha jumla ya alama 30 ikiwa nyuma alama moja kwa Simba.

No comments:

Post a Comment