Didier Drogba ameposti picha kupitia ukurasa wake wa Instagram iliyokuwa na ujumbe wa kumpa nguvu Lukaku baada ya kukosa penati katika mchezo wa fainali ya Super Cup.
Lukaku wa Chelsea akionekana kutahayari baada ya kukosa penati katika fainali ya Super Cup.
Lukaku akionekana ni mwenye huzuni akifarijiwa na wachezaji wenzake baada ya kukosa penati.
Mshambuliaji wa Chelsea Romelu Lukaku ambaye alikosa penati usiku wa jana dhidi ya Bayern Munich ambayo ilipelekea Munich kushinda taji la Super Cup amepozwa machungu na kutiwa moyo na mshambuliaji wa zamani wa The Blues Didier
Drogba.
Lukaku mwenye umri wa miaka 20 alishuhudia penati yake ikiokolewa na mlinda mlango wa Munich Manuel Neuer mjini Prague
ambayo iliwapa ubingwa ubingwa Munich ambayo haikuwa na bahati ya kufunga magoli katika muda wa kamwaida wa mchezo huo kabla ya kupata bao la dakika za majeruhi za muda wa nyongeza.
Lakini hata hivyo mshambuliaji nguli wa zamani wa Stamford Bridge Drogba, ambaye kwasasa anaichezea Galatasaray ya Uturuki ametoa maneno ya kumfariji Lukaku kwa kusema Mbelgium
huyo hapaswi kukata tamaa.
Drogba mshambuliaji wa kimataifa wa Ivory Coast ambaye ameposti picha yake akiwa na Lukaku kupitia ukurasa wake wa Instagram ikiwa imeambatana na ujumbe
'Only those who don't take a penalty never miss and
you were strong enough to do it.
'You are learning, the same way I learnt with this red card in the final in Moscow or this semi-final against Barcelona!!!
'Keep on working hard better days are coming for sure. You are Chelsea, you're a blue and blues never give up.'
Drogba akiwa katika jezi ya timu yake ya sasa ya Galatasaray.
Mfumania nyavu Drogba akifurahia ushindi enzi zake akiwa na klabu yake ya zamani wa Chelsea.
No comments:
Post a Comment