MWENYEKITI
wa klabu ya Simba Ismail Aden Rage,amepinga agizo la Shirikisho la Mpira wa
Miguu nchini TFF, ambalo limemtaka kuitisha Mkutano Mkuu wa Wanachama kujadi
malumbano liyopo ndani ya timu hiyo.
Rage alisema
amesikitishwa sana na TFF, kutokana na maagizo hayo ya kumtaka aitishe mkutano
wakati kwa mtazamo wake alifikiri watakemea vitendo hivyo vya kufanya mapinduzi
ambavyo vimepitwa na wakati
“Siwezi
kuitisha mkutano kwa sababu kufanya hivyo ni sawa na kupokonywa na madaraka
yangu tena mbaya zaidi napangiwa hadi ajenda ya kuzungumza na endapo
TFF,watanilazimisha kufanya hivyo nitajiuzulu,’alisema Rage.
Rage alisema
kwenye katiba ya Simba ibara ya 28 kifungu cha kwanza (a),(b),(c) na (d)
inamtambua Mwenyekiti,Makamu Mwenyekiti na Wajumbe saba siyo Kaimu Mwenyekiti
ambaye hatambuliwi na Katiba hiyo wala ile ya TFF.
Rage alisema
Katiba ya Simba ibara ya (22)inasema Makamu Mwenyekiti wa Simba anatambuliwa
kihalali kwa kuchaguliwa kwa kupata kura 50 +1 na Mwenye Mamlaka ya kuitisha
Kamati ya Utendaji ni Mwenyekiti na siyo mtu mwengine.
“Kwa mujibu
wa vifungu hivyo Joseph Itang’are bado hajawa na uwezo wa kuitisha mkutano wa
Kamati ya Utendaji kwa vile hatambuliwi na Katiba ya Simba,”alisema Rage.
Mwenyekiti
huyo alisema kutokana na makosa yaliyofanywa na viongozi hao kwenye katiba ya
TFF,Ibara ya 73 adhabu za viongozi hao ni kufungiwa kwa miaka 10 kutojihusisha
na maswala ya soka kwenye klabu husika.
Katika
mkutano huo Rage ameongelea mambo mengi ikiwemo tuhuma za kula pesa za usajili
wa mchezaji Emmanuel Okwi pamoja na fedha za udhamini wa Televisheni za ZUKU
TV.
Pia kiongozi
huyo alitumia mamlaka yake kama Mwenyekiti wa klabu ya Simba kumtangaza Michael
Richard Wambura kuwa Mjumbe wa Kamati ya Utendaji huku aliyekuwa akishikilia
nafasi hiyo Rahma Al Kharoos akiteuliwa kuwa Mdhamini wa klabu hiyo na amefuta
mkutano wa Tarehe moja
Mapema wiki
iliyopita Kamati ya Utendaji ya klabu hiyo ilitangaza kumwengua Rage kwenye
nafasi yake ya Uwenyekiti na nafasi yake kukaimiwa na Joseph Itang’are, na
kuitaarifu TFF,ambayo nayo ilipinga mapindizu hayo na kumpa siku 14 kiongozi
huyo kuitisha mkutano ili kumaliza malumbano yao.
No comments:
Post a Comment