Wachezaji wa kikosi cha timu ya taifa ya Ethiopia jana wakifanya mkutano na waandishi wa habari walilazimika kuomba radhi mashabiki wa waungaji mkono wa timu ya taifa baada ya kurejea nchini Ethiopia
Ndani ya barua yao iliyosainiwa na wachezaji wote wa timu hiyo wachezaji hao wameomba radhi kutoka na kutoa matumaini makubwa kuwa kikosi chao kingeweza kufuzu kucheza kombe la dunia la fifa 2014 nchini Brazi lakini hatimaye wakashindwa kufikia matarajio.
Wameelezea juu ya changamoto walizokutana nazo wakati wa safari nzima ya kusaka nafasi lakini walishindwa kukabiliana nazo.
Wamewataka mashabiki wa soka nchini huko kusahau yaliyopita na kwamba waendeleea kuwaunga mkono na kutoa maelezo kuwa kwao hilo lilikuwa ni jaribio kubwa kuwahi kufanya la kucheza kombe la dunia na kuahidi wakati mwingine itakuwa ni zaidi ya hilo na hivyo watatimiza ndoto zao kuwa kweli na watafuzu kucheza kombe la dunia.
No comments:
Post a Comment