
Mohamed Bin Hammam mwenye umri wa miaka 61anaonekana kama ndiye mpindani mkubwa kwa mkongwe huyo toka Uswize licha ya taarifa za hivi karibuni kuarifu kuwa Bin Hammam hana mpango na kiti hicho.

Akikaririwa Bin Hammam anasema "I will not run for the next Fifa election. I will back Sepp Blatter to remain in office".
Lakini kama Bin Hammam atawania nafasi hiyo basi anatarajia kupata ushindani mkubwa kutoka kwa Rais wa sasa wa shirikisho la kandanda barani ulaya Uefa Michel Platini.

Bin Hammam ambaye pia ni mjumbe wa kamati ya utendaji ya Fifa anasema pia na yeye anatarajia kuingia katika kinyanganyiro kingine cha kuwania Urais wa shirikisho la kandanda barani Asia (AFC) mwakani.
Baada ya miaka 12 kukalia ofisi ya FIFA Kama Rais , Blatter ameweka wazi kuwa hana mpango wa kuondoka hiyo June 11 2011,huku akisema bado hajamaliza baadhi ya mipango yake.
Kwa mara ya kwanza kuchaguliwa katika shirikisho hilo ilikuwa ilikuwa ni mwaka 1998 na baadaye kushinda tena kiti hicho mwaka 2002 before kisha kufanya hivyo tena katika uchaguzi wa mwaka 2007.

Swali lililopo ni nani atachukua kipindi hicho kingine cha uongozi ndani ya Fifa?
Na je dunia ya kandanda iko radhi kumuachia kiongozi huyu?majibu juni mwakanni
No comments:
Post a Comment