KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Friday, August 27, 2010

JAN POULSEN ATANGAZA SILAHA ZAKE DHIDI YA ALGERIA KUELEKEA ALGERS KWA MCHEZO WA KWANZA
Kocha mkuu wa timu ya taifa ya tanzania "Taifa Stars" Jan Paulson ametangaza kikosi cha timu hiyo chenye jumla ya wachezaji 20 watakao ivaa timu ya taifa ya Algeria katika mchezo wa kwanza wa kuwania kufuzu kwa fainali za mataifa ya Afrika.

katika kikosi hicho jumla ya wachezaji saba watalazimika kusalia nyumbani kutokana na sababu ambazo kocha huyo alizo ziita kuwa ni kutokuwa fiti kwa wachezaji hao.Wachezaji walioachwa ni pamoja na Juma Kaseja,Uhuru Selemani,Jerison Tegete,Kelvin Yondani,Abdulhalim Humoud,Athumani Iddi Chuji pamoja na Juma Jabu.

Poulsen ametoa sababu nyingine za kuwaacha baadhi ya wachezaji kuwa ni pamoja na namna ya uchezaji ya wachezaji hao akichukulia mfano wa baadhi ya wachezaji walipokuwa dimbani katika mchezo wa hivi karibuni wa kirafiki dhidi ya Kenya "Harambee Stars"kuwa kilikuwa ni kipimo cha kuamua nani kwasasa anaweza kuendana na kasi pamoja na mfumo wa uchezaji anaoutaka yeye.Hata hivyo amesema kikosi chake kiko fit kuivaa Algeria katika mchezo huo wa kwanza.

No comments:

Post a Comment