KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Friday, August 27, 2010

TASWA KUMPATIA TUZO RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE
Juu katika picha kutoka kushoto katibu wa TASWA Amir Mhando,mwenyekiti wa TASWA Juma Pinto na makamu mwenyeti wake Maulid Kitenge wakiongea na waandishi wa habari
Chama cha waandishi wa habari za michezo nchini TASWA kimeandaa tuzo maalum kwa ajili ya kumtunuku Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete kufuatia mchango wake katika kuendeleza sekta ya michezo nchini.
Hatua imekuja kufuatia Rais Kikwete kufanya jitihata za makusudi kuendeleza michezo na burudania hapa nchini .tayari Rais kikwete amefanikisha ujio wa makocha wa kigeni wa michezo kadhaa ikiwa ni pamoja na soka, ngumi na judo huku pia akiwa na dhamira ya kuhakikisha kuwa mchezo wa riadha na mpira wa pete nayo inapata waalimu wakigeni wenye uwezo wa kukuza viwango vya michezo hiyo hapa nchini.
Katika hatua nyingine TASWA imejipanga kuweza kutoa semina za mara kwa mara kwa waandishi wa habari za michezo hapa nchini ili kuwapa uwezo wa kuandika habari za michezo kwa usahihi.

No comments:

Post a Comment