KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Monday, August 16, 2010

KATIKA TENNIS MAMBO YA TORONTO SASA KAZI NI FEDERER DHIDI YA MURRAY PATACHIMBIKA Federer amtoa Djokovic,sasa kukutana na Murray katika fainali
kama Andy Murray anataka kurejesha haeshima aliyoipata katika kutwaa taji la Rogers Cup atalazimika kumchapa Roger Federer.

Federer amefanikiwa kuingia katika fainali iliyofanyika jumamosi dhidi ya Novak Djokovic kwa ushindi wa seti 6-1, 3-6, 7-5 wakati ambapo Murray amefanikiwa kuchapa mkali anayeshikilia nafasi ya kwanza kwa ubora duniani Rafael Nadal 6-3, 6-4 katika nusu fainali ya kwanza.

Murray na Federer watakuwa wakikutana kwa mara ya kumi na moja huku Murray akifanikiwa kumshinda Federer mara sita .kwa mara ya mwisho Federer alimshinda Murray walipokutana katika Australian Open na katika historia yao amefanikiwa kumshinda mara tatu katika fainali ya michuano mbalimbali .

Murray anatafuta kuwa mwanaume wa kwanza kurejea kushinda taji la Rogers Cup tangu kwa mara ya mwisho kufanywa hivyo na Andre Agassi mwaka 1995.

Ushindi wa Federer dhidi ya Djokovic maana yake ni kwamba unamrejesha katika nafasi ya 2 kwa ubora huku Djokovic akielekea katika nafasi ya 3

No comments:

Post a Comment