KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Wednesday, September 15, 2010

Nyota wa Man Utd Antonio Valencia sasa kumalizia msimu nje ya dimba baada ya kuvunjika mguu
Nyota wa mashetani wekundu Manchester United Antonio Valencia kuna uwezeknao mkubwa wa kuwa nje kwa msimu mzima baada ya ya kukumbwa na majeraha makubwa ankle ambayo yanasadikika kuwa ni makubwa majreha ambayo yametokana na mchezo wa jana wa ligi ya mabingwa ulaya dhidi ua Rangers mchezo ambao ulimalizika kwa sare ya bila mabao .
Winga huyo alikutana na tackling ya aina yake toka kwa Kirk Broadfoot mnamo dakika ya 62 ya mchezo .
Valencia mwenye umri wa miaka 25 lipelekwa hospitali na alitaarajiwa kufanyiwa upasuaji hii leo .
Akikaririwa meneja wa kikosi cha united Alex Furguson anasema
"inaonekana amepatwa na hali mbaya huenda akawa nje kwa kipindi kirefu hata msmu mzima."
Ferguson amelinganisha matatizo yake na mchezaji wake wa zamani Alan Smith ambaye alivunjika mguu katika michuano ya FA dhidi ya Liverpool mwezi February mwaka 2006.
Smith alikwenda nje ya dimba kwa takribani miezi saba matatizo ambayo yanaatazamwa kufananishwa na hili la Valencia ambaye huenda akawa nje ya dimba mpaka April mwakani.
Ferguson ameonyesha kusikitishwa kwake na hali ya Valencia na kuongeza
"ni pigo kubwa kwa kijana wake huyo lafanana na la Alan Smith.
Majeraha ya Valencia pia yamemuhuzunisha Darren Fletcher na kutabiri kuwa nyota huyo wa Ecuador atakuwa katika kipindi kirefu Old Trafford.
Majeraha ya Valencia pia yamefananishwa na mcheza rugby wa uingereza Danny Cipriani mwezi May 2008.
Cipriani alikubwa na “fracture dislocation” yaani kuachana kwa mifupa maumivu ambayo yalimuweka nje ya mchezo huo kwa miezi mitano.

Mshambuliaji wa zamani wa Arsenal Eduardo alivunjika mguu kama hivyo katika mchezo wa ligi kuu ya uingereza dhidi ya Birmingham mwaka 2008 kiasi kuchelewa kurejea dimbani kwa muda mrefu.
Maumivu ya Valencia yanaongeza majeraha ndani ya klabu hiyo kufuatia Michael Carrick kuwa nje ya dimba kutokana na maumivu ya ankle licha ya mbarazil Anderson kuwa tayari kurejea dimbani baada ya kuwa nje ya dimba kwa miezi saba kufuatia maumuvu ya msuli.
Hata hivyo Ferguson ana wachezaji wengine katika benchi ambao wako fomu akiwemo Nani, Gabriel Obertan,mkongwe Ryan Giggs ambaye alichukua nafasi ya Valencia usiku wa jana na Ji-Sung Park ambaye alinza katika upande kushoto katika mchezo wa kundi la C dhidi ya mabingwa wa Scottiland .


Aston Villa yathibitisha Gerard Houllier kuanza kazi baada ya mchezo wa jumamosi dhidi ya aston villaAston Villa yathibitisha Gerard Houllier kuanza kazi
Meneja mpya wa Aston Villa Gerard Houllier anatarajiwa kuchukua nafasi ya kuanza kuifundisha timu baada ya mchezo wa nyumbani dhidi ya Bolton jumamosi hii kwa mujibu wa taarifa ambazo zimethibitishwa na klabu hiyo.
Houllier alitajwa kama bosi mpya wa Villa juma lililopita lakini amekuwa katika subiri ya kuwekwa sawa kwa mambo yake ya ukurugenzi wa ufundi wa shirikisho la kandanda la ufaransa.
Mchezo wa kwanza wa Houllier utakuwa ni wa michuano ya Carling Cup dhidi ya Blackburn September 22.
Houllier amechukua nafasi ya Kevin MacDonald ambaye ataendelea kukalia benchi la ufundi katika mchezo dhidi ya Bolton.
Houllier mwenye umri wa miaka 63 ameingia mkataba wa miaka mitatu na Villa lakini bado kuingia makubaliano ya tarehe ya kuondoka na shirikisho la kandanda la ufaransa FFF tangu alivyothibishwa kwenye vyombo vya habari wiki iliyopita.

UINGEREZA YAPANDA MPAKA NAFASI YA SITA KATIKA VIWANGO VIPYA VYA UBORA WA KANDANDA VYA FIFA HUKU TANZANIA IKIPANDA KWA NAFASI MOJA NA KUSHIKA NAFASI Y 111


Matokeo mazuri ya timu ya taifa ya uingereza katika mchezo ya kuwania kufuzu kwa fainali za kombe la EURO 2012 kumeiisaidia kuweza kufanya vizuri katika ubora wa kandanda lake dunia baada ya kuchumpa mpaka katika nafsi ya 6 katika viwangi vya dunia.
Hispania ambao ndio mabingwa dunia wameendelea kusalia katika nafasi ya kwanza mbele ya uholanzi huku ujerumani ikikamata nafasi ya tatu na kufuatiwa na Brazil katika nafasi ya nne na Argentina ikikamata nafasi ya tano.
Jamuhuri ya Ireland imepanda kwa nafasi tatu na kujikita katika nafasi ya 33rd,huku majirani zao wa jamuhuri ya Ireland ya kaskazini ikijiweka katika nafasi ya 45 ikipanda kwa nafasi 14 Scotland nafasi ya 47 na Wales ikishika nafasi ya 84.
Ufaransa ambayo imekuwa na matokeo mabaya imeteremka mpaka mpaka nafasi ya 27.
Kufuatia dhahama ya ya matokeo mabaya ya kombe la dunia kocha mpya wa ufaransa Laurent Blanc na kikosi chake cha ufaransa 'walijikuta katika wakati mgumu katika mchezo wa awali wa michezo ya kufuzu fainali mataifa ya ulaya kwa Belarus licha ya kupata ushindi katika mchezo dhidi ya Bosnia.
Uingereza kama ilivyokuwa kwa wafaransa nao walikuwa katika hali mbaya katika fainali za kombe la dunia nchini afrika kusini lakini wamekuwa katika faraja ya kimatokeo katika michezo ya kufuzu ulaya baada ya kupata matokeo ya kuridhisha.
Kikosi cha Fabio Capello kiliichapa Bulgaria kwa jumla ya mabao 4-0 na kisha kuichapa Switzerland kwa jumla ya mabao 3-1 mapema mwezi huu.
Fifa imerekebisha viwango vyako baada ya michezo ya michezo ya hivi karibuni katika jumla ya michezo ya kimataifa 159 iliyopigwa hivi karibuni katika kipindi cha wiki tano.
Michezo ya Euro 2012 na ile ya kufuzu mataifa ya afrika 2012 Africa Cup of Nations ndiyo iliyo iliyopewa kipaumbele.
Fifa world rankings:
1 Spain
2 Netherlands
3 Germany
4 Brazil
5 Argentina
6 England
7 Uruguay
8 Portugal
9 Egypt
10 Chile
Mabadiliko makubwa ni kwa mataifa ya
Republic of Ireland 33
Northern Ireland 45
Scotland 47
Wales 84


barani afrika Misri ama Egypt imeendelea kushika uongozi wa ubora barani afrika na kufuatiwa na Ghana Ivory coast wakishika nafasi ya tatu huku Nigeria ikishika nafasi ya nne na nafasi ya tano ikishikiliwa na Algeria.Gabon wako katika nafasi ya sita ilhali Camerron wakishika nafasi saba na kufuatiwa na Bukina faso Mali na Benin katika nafasi za nane tisa na kumi

Upande wa Afrika mashariki na kati Uganda wameongoza kwa kushika nafasi ya 13 barani Afrika na ikishika nafasi ya 69 na kufuatiwa na Tanzania iliyo katika nafasi ya 27 kwa bara la Afrika huku duniani ikishika nafasi ya 111.

kenya wako katika nafasi ya 31 barani Afrika ilhali dunia ikishika nafasi ya 113.Sudan iko katika nafasi ya 32 barani Afrika huku dunia ikishika nafasi ya 120 ilhali Burundi wakiwa katika nafasi ya 37 barani Afrika na kwa dunia ikishika nafasi ya 142.Rwanda ikiishika koo Tanzania kwa kukaribiana wakishika nafasi kama ya Tanzania ya 28 barani Afrika lakini duniani wakiwa na alama sawa 235

No comments:

Post a Comment