KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Thursday, October 28, 2010

MFAHAMU GREGORY ISSACK ALIYEFARIKI DUNIA AKIWA NA UMRI WA MIAKA 59


Gregory Isaacs aliyekuwa na umri wa miaka 59, na mwimbaji wa muziki aina ya reggae mzaliwa wa Jamaica akijulikana zaidi kama “cool ruler” kwa aina yake ya uimbaji maarufu kama “lover’s rock” amefariki dunia kutokana na matatizo ya kansa ya ini akifariki October 25 nyumbani kwake huko London .

Tofauti na waimbaji wengine wa reggae wa aina ya musik wa “roots rock” kama vile marehemu Bob Marley na Burning Spear ambao pia walijulikana sana kwa kuimba nyimbo siasa ya dunia na utamaduni wa ki-Rastafarian Gregory Isaacs alijulikana zaidi kwa nyimbo zake mapenzi alizo ziandika.

Mtindo wa uimbaji wa kubembeleza na mara kadhaa akiimba kwa kuomba mapenzi na kuwataka wapenzi kumuelewa.mara kadhaa alikuwa akionekana amevalia kofia kama maarufu hapa nchini kama ma lakini kwingineko alitambulika kama “fedora” na akitinga jackets dogo unaweza sema kama la kitoto, Mr. Isaacs alionyesha mchanganyiko wa mahadhi ya uimbaji licha ya kwamba akituama kwenye ala za reggae alikuwa akiwachanganyaka mashabiki wake kiasi kumlinganisha na waimbaji wa musiki laini toka nchini Marekani hawa nia akina Tyrone Davis na Marvin Gaye.

Mwandishi wa gazeti la New York Times ambaye pia amekuwa mkosoaji mkubwa wa musiki alimwita Gregory Isaacs "the most exquisite vocalist in reggae,"yaani ni mwimbaji mwenye kipaji cha ina yake na mwenye kukonga nyoyo kwa sauti katika musiki wa reggae "nyimbo zake za kimapenzi zenye hisia za mahaba si tu za kimapenzi lakini pia zinauwezo wa kubembeleza ndani ya usingizi wa mchana na zisizo mchosha msikilizaji"

Wimbo wake uliopatia mafanikio makubwa ni "Night Nurse"alio utoa mwaka 1982 ulishika na kuikamata dunia .

"Night Nurse," ukiwa na mashairi safi huku sehemu tu ya mistari ikisema "I don't wanna see no doc. I need attendance from my nurse around the clock. There's no prescription for me, she's my only remedy" ulichukua nafasi katika majumba ya starehe mwaka huo wa 1982 na kumtambulisha vizuri Isaak.

Mwaka huo huo wa 1982 Gregory Isaack alikakatwa na kutupwa jela kwa miezi sita kwa shitaka la kumiliki silaha ya moto yaani bunduki kinyume cha sheria.
Hata hivyo mwenyewe alitumia muda mwingi kujitetea akisema alimiliki bunduki hiyo ili kujilinda na wahuni na ghasia za kisiasa ambazo ziliigubika mwishoni mwa miaka ya 1970 na akisema alifanya hivyo kujilinda kama mtu yoyote anavyoweza kujilinda na baridi kwa kuvaa jacket

Baadaye ikaripotiwa kuwa Gregory Isaack ameweza kwenda ndani mara 27 na mara kadhaa akituhumiwa kwa makosa ya kujishughulisha na madawa ya kulevya ukweli ambao baadaye ilibidi atafutwe kwa ajili ya kufanyiwa mahojiano .

Gregory Anthony Isaacs alizaliwa July 15, 1951 katika eneo la Denham karibu karibu na kitongoji cha Kingston sehemu ambayo alikuwa akisikiliza sauti tamu ala za music laini za waimbaji wa kimarekani waliomvutia wakati ule kama vile Sam Cooke na Ben E. King.
Baada ya kushinda maonyesho mbalimbali ya vipaji akiwa kijana zaidi ndipo kwa mara ya kwanza akajikuta akiingia studio akijumuika na mkongwe Winston Sinclair mwaka 1968 na kuimba naye wimbo wenye jina la Concords ulioimbwa kwenye mahadhi ya rock.

Mwaka 1973 akachomoka kivyake na kuanzisha kampuni yake ya musiki iliyoitwa African Museum akiwa na jamaa mwingine mwimbaji toka Jamaican Erroll Dunkley.hapo waliibuka na nyimba kali kadhaa zilizotamba huko Jamaica kama "My Only Lover" (1973), na wimbo mwingine ulioonekana wimbo wa kwanza wa aina ya Rock "Love Is Overdue" (1974) na kisha akatoka na ngoma ya "All I Have Is Love" (1976).

Kampuni maarufu ya Island Records,ikaanza kutoka na nyimbo zake mbalimbali huko nchini marekani mnamo mwaka 1982. Gregory Isaacs alikuwa mtunzi na mwenye kazi nyingi sana za muziki kiasi kuarifiwa kupitia mtandao wa All Music Guide inakadiriwa ameshiriki karibu katika album 500 za wasanii mbalimbali wa Jamaica,Marekani na Uingereza

Isaacs ameshiriki kiasi katika moja ya filamu huko Jamaica iliyokwenda kwa jina la "Rockers," ya mwaka 1978 katika pia mchezo wa kuchekesha kwenye luninga ambao unatambulika kama "A Hard Days Night" inayo husisha muziki wa reggae. Ndani ya filamu hiyo alionekana kama fundi wa funguo ambaye alikuwa akibishana na watalii wawili ambao gari lao lilikuwa limejifunga kwahiyo walikuwa wakibisha juu ya malipo ya kazi hiyo na baadaye usiku wake akaonekana akiimba katika ukumbi wa yaani “night club”.

Katika uhai wake marehemu Gregory Isaacs alifunga ndoa na wanawake mara idadi ya watoto wake bado kuthibitishwa .

Aliendelea kufanya ziara za kimuziki mara kadhaa katika miaka ya 1990s.wakati hayo yakiwa hivyo mwaka 2007, gazeti la London Daily Telegraph liliarifu ya kuwa mkongwe huyo wa muziki wa reggae alianza kuathirika na matumizi kupindukia ya mihadarati aina ya cocaine kiasi kuanza kupoteza meno matatizo ambayo aliathiri kazi zake za uimbaji.

No comments:

Post a Comment