Venue:
Donbass Arena, DonetskDate: Saturday, 23
Kocha wa Hispania
Vicente del Bosque kwa mara nyingine tena anatarajia kuanzisha Fernando Torres katika
kikosi chake ambacho kimekuwa hakina mabadiliko.
Hii maana
yake atamuacha Cesc Fabregas katika benchi ambaye ana magoli mawili katika
michuano hii kama ilivyo kwa Fernando Tores.
Ufaransa
itakuwa dimbani hii leo bila ya mlinzi wa kati aliyesimamishwa Philippe Mexes kufuatia
kadi mbili za njano na badala yake Laurent Koscielny ataanza katika kikosi
hicho kwa mara ya kwanza.
Yohan Cabaye anatarajiwa kuanza baada ya kuponya majeraha yake yaliyopelekea kuukosa mchezo dhidi ya Sweden.
Samir Nasri na Franck Ribery wanatarajia kuwa fit katika kikosi cha Ufaransa kitakacho kabiliana dhidi ya Hispania hii leo.
Ananukuliwa kocha msaidizi wa Ufaransa Alain Boghossian akisema
"wanaendelea vizuri hawakufanya mazoezi jumatano katika kujaribu kuona wanaimarika"
No comments:
Post a Comment