mashabiki wa soka wa England mjini Kiev |
Mashabiki wa England mjini Kiev wakiwa pamoja na mashabiki wasichana wenyeji wa mjini
Kiev sasa wameungana na mashabiki wa England baada ya Ukraine kuondoshwa
mashindanoni
Polisi wasema
takribani mashabiki 6,000 wa England wanatarajiwa
kuwepo uwanjani katika mchezo war obo fainali ya mwisho ya Euro 2012 dhidi ya Italy.
British
Airways inatumia sasa zile ndege kubwa zaidi kuwasafirisha mashabiki kuelekea Ukraine
kuwawezesha mashabiki kuiona England ikicheza katika hatua hii ya robo fainali
ambayo nihatua ya mtoano.
Wakati wa
hatua ya makundi inakadiriwa mashabiki waliokuwa Ukraine walikuwa 3,000.
Afisa wa
polisi msaidizi Chief Constable Andy Holt mjini Ukraine anasema hakukuwa na
shabiki hata mmoja wa England aliyewekwa ndani katika kipindi hicho.
Mr Holt
anawakilisha Association of Chief Police Officers anasema
"tutakuwa
na maafisa wa polisi airport kujaribu kuwadhibiti mashabiki wakati wakiwasili
tuna maafisa wanaovalia uniform hapa katikati ya mji wa Kiev na nje
wakizungumza na mashabiki lakini pia kutakuwepo maafisa polisi wa Uingereza.
No comments:
Post a Comment